Mwanafunzi anayesomea udaktari
nchini Marekani ambaye alikuwa ana nadi ubikra wake, amesitisha shughuli
hiyo baada ya watu wachache sana kujitokeza wakiwa tayari kuulipia
ubikra wa mwanamke huyo.
Pamoja na hilo Kern hakua na uhakika kuhusu ukweli wa waliojitokeza kulipia ubikra wake.Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Daily Mail.
Mwanafunzi huyo, Hanna Kern alikuwa ana nadi ubikra wake chini ya jina ambalo sio lake 'Elizabeth Raine' kwa hofu ya watu kumtusi. Pia hakuweka sura yake kwenye mtandao hadi alipofanya mahojiano na jarida la Haffington post.
Kern ana umri wa miaka 28 na ana digrii ya uzamifu kutoka chuo kikuu cha Washington, nchini Marekani.
Kern ni mwanafunzi wa hivi karibuni aliyenadi ubikra wake kwenye mtandao bila matokeo aliyoyataka.
Hata hivyo alilazimika kuusitisha mnada wake baada ya kukosa kupata kima alichokitaka na hata pia kukosa kupata wanaume wengi waliovutiwa na kampeini yake na kuhofia kuwa waliojitokeza kuulipia sio watu wakweli.
Pia alieleza kuwa alisumbuka sana kiakili kutokana na umaarfu aliopata baada ya kufichua jina lake la kweli na kuonyesha sura yake.
Alikunukuliwa akisema baada ya kukosa kufanikiwa kupata hela alizozitarajia, hana wasiwasi na hilo kwani amapeta funzo na kujua kwa nini kampeini kama hizi huwa kazifanikiwi.
Wa mwisho aliyejitokeza kulipia ubikra wake alikuwa ametoa kima cha dola 801,000,lakini mwanafunzi huyo aliamua kutoendelea na juhudi zake kwani hakufurahishwa na pesa hizo.
''Nimeamua kusitisha kempeini yangu, na kurejea katika msomo yangu ya udaktari.''
''Bado ninaamini kuwa ubikra ni kitu kizuru na pia ninaamini kuwa mwanamke anapaswa kuachwa afanye anavyotaka, '' ingawa kwa sasa masomo ndio ninayotaka kushughulika nayo,'' alisema Kern.
No comments:
Post a Comment