Nape |
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
matokeo ya uchaguzi huo ambao umeonyesha kuvinufaisha vyama vya upinzani
kupitia umoja wao wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Nape alisisitiza kwamba makosa hayo ndiyo yaliyosababisha wapinzani kujinyakulia mitaa kadhaa kwa wepesi.
“Tumejifunza na tumekuwa tunajaribu kila wakati
kubadili mfumo wetu wa kura za maoni lakini bado kumekuwa na matatizo.
Kwa mfano, kuna Mtaa Mwenge Dar es Salaam, wanaCCM waliamua kumchagua
mgombea wa upinzani baada ya jina la waliyempenda kutorudi,” alisema
Nnauye na kuongeza:
“Tunajua kwamba kuna maeneo mengi ambayo wapinzani
wameshinda. Ukiangalia CCM tulifanya makosa katika kumweka mgombea,
hivyo kusababisha hasira ambazo kwa kweli zimewafurahisha wapinzani
lakini sisi zimetugharimu,” alisema.
Alisema chama chake kitafanya tathmini ili kubaini
kama sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow nalo ni miongoni mwa mambo
yaliyochangia kupoteza baadhi ya mitaa.
Hata hivyo, Nape alisema wapinzani hawapaswi
kuufurahia ushindi walioupata, bali iwe ni changamoto kwao katika
kuhakikisha wanawatumikia wananchi waliowaamini
No comments:
Post a Comment