Thursday, 4 December 2014

Lungu ndiye mgombea wa PF Zambia

Mahakama kuu nchini Zambia imetangaza kuwa waziri wa Ulinzi Edgar Lungu ndio atakeyewania wadhfa wa Urais kupitia tiketi ya chama cha Patriotic Front katika uchaguzi wa mwezi Ujao.
Chama cha Patritic Front kimegawanyika kuhusu ni nani atakayekrithi rais sata kufuatia kifo chake.
Mgawanyiko huo utafungua njia kwa upinzani kuchukua mamlaka katika uchaguzi huo kulingana na wachambuzi.
Makundi pinzani ya chama cha PF yalifanya mikutano tofauti katika kipindi cha juma moja ili kumchagua mgombea wa urais katika uchaguzi huo wa january 20.
Upande wa bwana Lungu ulipinga uteuzi wa Bwana Sampa mahakamani.
''Mkutano wa chama unaodaiwa kufanyika Disemba mosi ambapo mheshimiwa Miles sampa anadaiwa kuchaguliwa kama mgombea wa chama cha Patritic Front nataka kutangaza kwamba ni haramu na uamuzi wote ulioafikiwa si wa halkali'',Jaji aliamuru.
Kaimu rais wa Zambia Guy Scott
Bwana sampa amesema kuwa atakataa rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Kiongozi huyo ni mshirika wa karibu wa kaimu rais Guy Scott ambaye alichungua mamlka baada ya kifo cha Sata katika hospitali ya Uingereza mnamo mwezi Octoba akiwa na umri wa miaka 77.
Bwana Scott alichukua jukumu muhimu katika mgogoro wa kuwania mamlaka alipomuondoa kwa mda bwana Lungu kama katibu mkuu wa chama hicho mda mchache baada ya kifo cha Sata.
Hatahivyo alilazimika kurudisha bwana Lungu siku moja baadaye kufuatia lalama katika chama.
Bwana Scott ambaye hawezi kupigania urais anajaribu kuwa mtu muhimu katika siasa za taifa hilo kulingana na wachambuzi..

No comments: