Mzunguko wa 14 umekamilika kwa timu zote 20 za ligi kuu ya England kushuka viwanjani.
Chelsea,
wameendeleza wimbi la ushindi na kukataa katakata kuzipa nafasi timu
nyingine 19 kupunguza pengo la pointi lililopo kati yake na timu hizo.
Sergio Aguero, mchezaji wa Manchester City akishangilia moja ya magoli yake katika ligi kuu ya EnglandChelsea imeendelea kuwa na
tofauti ya pointi sita na Man City inayoifuatia baada ya kuirarua
Tottenham mabao 3-0, huku Manchester City yenye pointi 30 ikiisasambua
Sunderland magoli 4-1. Sergio Aguero ameifungia timu yake ya Manchester
City magoli mawili katika mchezo huo, huku Jovetic na Zabaleta kila
mmoja akifunga bao moja. Magoli ya Chelsea yamefungwa na Hazard, Drogba na Remy. Wachezaji wa Arsenal Santi Carzola akishangilia goli na Alexis Sanchez
Mchezo mwingine wa Jumatano
usiku, ulikuwa kati ya Arsenal na Southampton wanaoshikilia nafasi ya
tatu katika msimamo wa ligi kuu ya England. Mchezaji Alexis Sanchez
ndiye aliyekuwa shujaa na kuwanyanyua vichwa mashabiki wa Arsenal pale
alipoifungia timu yake goli pekee katika mchezo huo ikiwa ni dakika ya
89 ya mchezo, uliofanyika uwanja wa Emirates na hivyo kujikusanyia
pointi tatu muhimu kuelekea kileleni.Arsenal inashikilia nafasi ya sita
ikiwa na pointi 23, pointi 13 nyuma ya vinara Chelsea yenye pointi 36.
Everton na Hull City ziligawa pointi baada ya kufungana bao 1-1.
Hadi
kufikia mzunguko huo wa 14, Chelsea inaongoza kwa kujikusanyia pointi
36, ikifuatiwa na Man City yenye pointi 30, Southampton ni ya tatu na
pointi 26, Huku Manchester United kiwa nafasi ya nne na pointi 25 na
nafasi ya tano inashikiliwa na West Ham yenye pointi 24.Ivabaada
No comments:
Post a Comment