Manchester United wanataka kuendelea kuimarisha kikosi chao kwa kumsajili winga Gareth Bale, mwenye miaka 25, toka klabu ya Real Madrid kwa dau la £90milion, pesa za mauzo ya Bale zitatumika kuwasajili nyota Eden Hazard wa Chelsea na kinda wa Liverpool Raheem Sterling.
Kocha wa zamani wa Liverpool Gerard Houllier, ambae kwa sasa ni mkurugenzi wa michezo wa timu ya New York Red Bulls yuko tayari kumpa ofa kiungo Steven Gerrard kujiunga na miamba hao wa ligi ya Marekani.
Manchester City imeingia katika vita na timu ya Manchester United katika mbio za kuwania saini ya mlinzi kisiki Mats Hummels, wa klabu ya Borussia Dortmund,Man City wako tayari kutoa kitita cha £47milioni ili kumtwaa mchezaji huyo.
Klabu yaTottenham wanafanya jitihada za kumsajili mshambuliaji Eran Zehavi, toka timu ya Maccabi Tel-Aviv inaaminika mchezaji huyo anapatika kwa kwa dau la £1.6milioni. Tottenham wanataka kuondoa tatizo la safu ya ushambuliaji inayoshindwa kufanya vizuri msimu huu.
Beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher amewataka Reds na meneja Brendan Rodgers kutoa £ 20milioni kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Wilfried Bony mwenye 26, toka Swansea katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.
Inter Milan wanapigana vikumbo na Ajax pamoja naReal Sociedad kuwania kupata nafasi ya kumchukua kwa mkopo winga kinda Adnan Januzaj. Manchester United wako tayari kumuachia winga huyo mwenye miaka19, akapate uzoefu Zaidi baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
No comments:
Post a Comment