Tuesday, 2 December 2014

Misri yafunga mipaka yao

Misri yafunga lango la mpakani tena
Misri imefunga lango la mpaka wa Rafah unaounganisha nchi hiyo na Gaza
Katika maelezo yaliyoandikwa na Kamati Kuu ya Mipaka na Milango ya mpakani, inayohusishwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya serikali ya Palestina iliyoko Gaza, iliarifiwa kwamba serikali ya Misri ilifunga lango la mpaka wa Rafah hadi amri ya pili itakapotolewa baada ya Wapalestina 554 waliokwama nchini humo kuvuka Gaza.

Viongozi wa Misri waliwahi kufungua lango la mpaka wa Rafah pia siku ya jumatano iliyopita kwa ajili ya Wapalestina waliokuwa wakisubiria kupita Gaza.

Kutokana na vizuizi vya Israel, ‘’Lango la Pekee la Gaza kwa dunia’’ la Rafah limekuwa likifungwa mara kwa mara baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyotekelezwa mwezi Julai 2013 nchini Misri. Hatimaye mnamo tarehe 24 Oktoba, baada ya mashambulizi kutekelezwa katika vituo 2 vya usalama mkoani Sinai Kaskazini, serikali ya Misri ilitoa ilani ya dharura ya miezi 3 kwenye eneo hilo kwa madai ya ‘’kutatua mizizi ya tatizo la ugaidi’’, na kuchukua hatua ya kufunga lango la mpaka wa Rafah katika mchakato huo.

No comments: