Mtanzania aishie Marekani ameshtakiwa kwa kuhusika katika njama ya
kimataifa ya kuingiza heroin nchni humo kutoka Tanzania. Mamlaka husika
huko Marekani wamemtaja Mtanzania huyo kuwa ni Allen Jordan Baisi (34)
na anahusika kwenye mtandao wa kimataifa wa kuingiza madawa ya kulevya
Marekani kwa kutumia vifurishi vinavyotumwa kutoka Tanzania kwenda kwa
"wateja" mbalimbali Marekani.
Hata
hivyo, "wateja" hao walikutwa kuwa ni wasaidizi wake wakuu katika
biashara yake haramu ya heroin. Kwa mujibu wa nyaraka za kimahakama,
mtandao wake unajumuisha kusafirisha heroin iliyofichwa ndani ya soli za
makubadhi (sandals) kwenye vifurushi vilivyokuwa vinatumwa kutoka
Tanzania kwenda kwenye anwani za nyumbani zilizoko katika kaunti ya
Muskegon.
Kwa mujibu ya wa tovuti ya mlive.com, Allen Jordan Baisi, ambaye anaishi
Mount Prospect, Ill, alikamtwa huko Illinois na kushshtakiwa mwezi
Octoba mwaka huu kwa kosa la kujihusisha kusambasa karibu gramu 100 za
heroin na kosa la money laundering. Kwa mujibu wa nyaraka za kimahakama,
Allen Jordan Baisi, ni Mtanzania na alikamatwa kwenye trafiki September
22 mwaka akiwa njia kuelekea uwanja wa ndege kuja Tanzania. Kesi yake
itaanza kusikilizwa Januari 6, 2015.
Bw. Baisi anashtakiwa pamoja na watuhumiwa wengine ambao wanajulikana
kwa majina na wengine hawajulikani. Waendesha mashtaka wanadai kuwa
heroin ilikuwa inafichwa kwenye vifurishi vya nguo ambavyo vilikuwa
zinatumwa kwenye anuani za nyumbani zilizopo katika kaunti ya Muskegon
na kuwa mtu mwingine ambaye nyaraka za kimahakama zinamtambulisha kama
"Individual A” alikuwa anapokea heroin hiyo na kuisambaza eneo hilo. Mtu
huyo alikuwa anakusanya malipo kutoka kwa wateja na kuyawasilisha kwa
Bw. Baisi huko Illinois ambaye alikuwa anazituma Tanzania na kubakia na
nyingine.
Mwaka 2013 na 2014, Bw. Baisi alipokea fedha kama malipo halafu
akazituma jiji Dar Es Salaam kama malipo ya alikonunua heroin hiyo. Kwa
mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Homeland Security ya Marekani kwenye
simu mbili za Bw. Baisi Ocktoba 7 mwaka huu baada ya kukamatwa,
mtuhumiwa aligundulika kuwa kwenye sehemu ya mtandao wa kimataifa wa
biashara ya heroin na money laundering kati ya Tanzania na Marekani.
Kwa mujibu wa ripoti ya Homeland Security, wanachama wa mtandao huo
wanaishi sehemu mbalimbali duniani zikiwemo Tanzania, India, kaskazini
mwa Illinois and magharibi mwa Michigan. Bw. Baisi anadaiwa kusimamia na
kufuatilia kwa njia ya kieletroniki jinsi vifurishi hivyo vilivyokuwa
vinasafirishwa kutoke Tanzania hadi Muskegon.
Mamlaka husika zilishtukia biashara hiyo ovu Disemba 2013 baada ya
kukamata vifurishi viwili (Express Mail parcels) vilivyokuwa vimetumwa
kwa wakazi wawili katika eneo la Muskegon. Kila kifurishi kilikuwa na
karibu gramu 150 za heroin iliyokuwa imefichwa ndani ya soli za sandals.
Uchunguzi ulidumu kwa miezi kadhaa kabla ya kukamata kifurishi cha tatu
chenye heroin July 2014 katika uwanja wa John F. Kennedy Airport jijini
New York kilichokuwa kinaenda katika anwani iliyopo magharibi mwa
Illinois iliyokuwa na uhusiano na Bw, Baisi.
Baisi alikuwa bado anatumikia kifungo cha nje tokea mwaka 2009 baada ya
kufungwa kwa kosa la kujihusisha na biashara ya heroin. Agosti 5 mwaka
huu, Polisi walimhoji Baisi nyumbani kwake Illinois. Inadaiwa kuwa
katika mahojiano hayo, Bw. Baisi alikiri kujihusisha katika mtandao wa
biashara ya madawa ya kulevya na money laundering kati ya Tanzania na
Marekani.
Baada ya Bw. Baisi kushirikiana na polisi waliokuwa wanafanya uchunguzi,
ikiwa ni pamoja na kuwakabidhi simu zake Augosti 25, polisi walipokea
taarifa Septemba 19 kuwa angeweza kuondoka Marekani Septemba 22. Maafisa
wa Customs waliidhibitishia polisi kuwa Baisi alikuwa amepanga kuondoka
na ndege ya Emirates kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O.Hare
kwenda Dar Es Salaam, Tanzania, kinyume na makubaliano ya yeye kutumikia
kifungi cha nje.
Baada ya kuambiwa hivyo, polisi walipata warrant na kumkamata Septembe
22 kwenye taa za trafiki maeneo ya Mount Prospect wakati akielekea
uwanja wa ndege kurudi Tanzania. Oktoba 30, mahakama iliamua kumweka
ndani bila bail kusubiri kesi yake. Jaji alisema Baisi ametenda kosa
ambalo adhabu yake ni si chini ya miaka 10 jela na kwamba kuna uwezekano
kuwa Baisi angeshindwa kutokea mahakamani au kuhatarisha maisha ya mtu
mwingine au jamii kama akiachiliwa.
No comments:
Post a Comment