Friday 19 December 2014

Haruna Moshi Kulipwa na Diamond

NYOTA wa zamani wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’, ambaye kwa sasa anakipiga Friends Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, atakuwa akilipwa mshahara wake na watu watatu akiwemo mwanamuziki Diamond Platinum.
Boban amesajiliwa katika timu hiyo baada ya kushindwana na Mbeya City dakika za mwisho za dirisha dogo ambapo   atakuwa analipwa Shilingi laki nane.
Mmoja wa viongozi wa Friends Rangers, alisema kwamba Diamond atakuwa anatoa Shilingi laki nne, kuna mdau mwingine ambaye hakutaka kutajwa jina lake atakuwa anatoa Shilingi laki tatu, huku wananchi wanaopenda timu hiyo watakuwa wanatoa Shilingi laki moja.
“Daimond amekuwa akimkubali sana Boban na amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha anarejea uwanjani kwa kasi ndio maana ameamua kujitolea kwa kutoa mshahara wake nusu,” alisema kiongozi huyo.
Katika mechi yao ya juzi waliyoicheza Uwanja wa Makurumla uliopo Magomeni Mwembe Chai, Dar es Salaam, dhidi ya Ruvu Shooting ambapo walishinda bao 1-0, Diamond alitoa Shilingi laki tano kama kuwatia moyo kujituma kwa bidii wakati wote wa mechi hiyo iliyokuwa ya kuvutia.

No comments: