Tuesday 2 December 2014

Mapambano dhidi ya Ebola yaonyesha kufanikiwa

Medical staffShirika la afya duniani WHO liemesema kiasi ya watu 6,000 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola katika nchi zilizoathirika magharibi mwa Afrika na sio 7,000 kama ilivyokuwa imeripoti hapo awali.
WHO imesema hitilafu ilitokea katika kuhesabu idadi ya vifo nchini Liberia.Shirika hilo la afya limesema limeshuhudia kuimarika kwa juhudi za kupambana na janga hilo ambalo limeziathiri vibaya nchi za Liberia,Sierra Leone na Guinea katika kupunguza maambukizi kwa kuwatenga wagonjwa na kuwazika kwa njia inayostahili waliokufa.Hata hivyo naibu wa katibu mkuu wa WHO Bruce Aywald amesema itakuwa changamoto kufikia lengo la asilimia 100 kuwatenga waathiriwa na kuwazika salama ifikapo tarehe mosi mwezi Januari na kuonya pia kumekuwa na kuzembea katika juhudi zinazopigwa nchini Liberia.

No comments: