Chama
cha Soka nchini Uingereza, kimemfungia mchezo mmoja, mshambuliaji wa
Liverpool, Mario Balotelli ikiwa ni adhabu kutokana na kile Super Mario
alichokiandika katika mitandao ya habari ya kijamii.
Adhabu
hiyo itamlazimisha nyota huyo wa Italia, kukosa mchezo wakati timu yake
ya Liverpool itakapoikaribisha Arsenal Jumapili, katika michezo ya ligi
kuu ya England. Pia amepigwa faini ya pauni£25,000 na lazima ahudhurie
kozi ya elimu.
Baloteli mwenye umri wa miaka 24 ameadhibiwa kwa mujibu wa sheria za FA kwa kutuma ujumbe ambao umeonekana kuwa na ubaguzi.
Balotelli amekubali adhabu hiyo lakini ameiandikia FA ili iweze kumpunguzia.
Baada ya
kujua adhabu yake, aliandika katika ukurasa wake rasmi wa Facebook
kwamba uamuzi wa FA "umeonyesha wazi" kwamba ujumbe wake ulikuwa
"makosa".
Balotelli
aliituma picha iliyotolewa na mtu mwingine tofauti. Alisema:
"nasikitika kwamba wachezaji wenzangu na mashabiki wa Liverpool FC
wataadhibiwa kwa kosa ambalo nimelifanya na sasa najutia. Ni dhamira
yangu kukubaliana na uamuzi wa FA na kuhakikisha kuwa halitatokea tena."
Msemaji
wa Liverpool amesema: "klabu inatambua uamuzi uliofikiwa na jopo huru la
FA na utapewa uzito unaostahili mara tutakapoupokea kutoka FA.
"Hatua yoyote itakayochukuliwa nasi kuhusiana na jambo hili itakuwa kati ya klabu na mchezaji."
Mchezaji
huyo wa zamani wa Manchester City Balotelli alirudia kutuma picha ya
mchezo wa kompyuta yenye kibonzo cha Super Mario katika mtandao wa
Instagram ambacho kilikuwa na maneno "ruka kama mtu mweusi na kusanya
sarafu kama myahudi."
Baadaye alituma ujumbe wa tweeter akikanusha kuwa ujumbe huo ulikuwa na makosa, kabla ya kuomba radhi.
Balotelli
alirejea katika kikosi cha Liverpool kilichocheza na Manchester United
katika uwanja wa Old Trafford Jumapili baada ya kukosa michezo sita
kutokana na maumivu ya nyama za paja. Katika mchezo huo Liverpool
iliambulia kipigo cha magoli 3-0.
Balotelli
ameifungia magoli mawili timu yake katika mechi 15 alizoichezea timu ya
Liverpool tangu atoke AC Milan msimu uliopita wa kiangazi

No comments:
Post a Comment