Mwanamuziki
mwenye sifa kedekede nchini Tanzania, Naseeb Abdul, kwa jina lengine,
'Diamond Platnumz', anaendelea kujizolea sifa kimataifa baada ya
kushinda tuzo tatu za Channel O African Music Awards.
Tamasha lilifanyika nchini Afrika Kusini mwishoni mwa wiki.Diamond alijizolea tuzo tatu, ikiwemo ya mwanamuziki mgeni mwenye kipawa kikubwa, mwanamuziki bora zaidi kwenye mtindo wa Afro-Pop na tuzo ya mwanamziki bora zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki.
Diamond anajulikana kama mwanamuziki anaeenziwa zaidi nchini Tanzania na alishinda tuzo hizo kwa wimbo wake 'Number One', na kuwabwaga wanamuziki wengine wanaosifika kikanda na kimataifa.
Hii ni mara ya pili mwaka huu kwa Diamond ambaye mwezi Mei alishinda tuzo saba katika mashindano mangine ya wanamuziki ikiwemo mwanamuziki bora zaidi wa kiume , mwandishi na mtunzi bora zaidi wa nyimbo pamoja na mtumbuizaji bora zaidi Tanzania.
Mwanamuziki Tiwatope Savaga wa Nigeria naye alijinyakulia tuzo ya mwanamuziki bora zaidi wa kike hasa kwa vile alivyoimba kibao chake 'Eminado'.
Tuzo hizo huandaliwa na kituo cha televisheni ambacho hucheza tu muziki cha Channel O.
No comments:
Post a Comment