Wapiganaji wazidi kushambuliana nchini Libya tangu kuanguka kwa utawala wa Muamar Gadaffi
Shambulizi
lililolenga kituo muhimu cha mafuta mashariki mwa Libya halikufua dafu
kutokana na mashambulizi ya angani yaliotekelezwa na vikosi vya serikali
vinavyotambuliwa kimataifa.
Kamanda
mmoja wa jeshi la wanahewa anasema kuwa mashambulizi ya angani
yaliwalenga watu wenye silaha waliokuwa wakisonga mbele katika kituo cha
mafuta cha Al-Sidra ambapo watu wengi waliuawa.
Zaidi ya miaka mitatu tangu kuanguka kwa utawala wa kanali Muamar Gadaffi serikali hasimu bado zinapigania madaraka nchini LibyaSource: BBC
No comments:
Post a Comment