Thursday 29 December 2016

Afariki dunia baada ya nyoka wake aliekuwa amembeba kuuawa.

Mkazi wa Mtaa wa Mateka, Manispaa ya Songea, Denis Komba (26) amefariki baada ya nyoka wake aliyekuwa amembeba kwenye mfuko wa jaketi kuuawa na wananchi.
Komba alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma (Homso) ambako alilazwa baada ya watu wenye hasira kumuua kwa mawe na fimbo nyoka wake huyo.
Mashuhuda wanaeleza kuwa kabla ya wananchi kumuua nyoka huyo, Komba aliwasihi wasifanye hivyo kwa kuwa wakimuua na yeye angekufa, lakini ombi lake hilo halikusikilizwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, siku ya tukio Komba alikodi pikipiki ya Kassian Haule (24) ambaye ni mkazi wa Mpitimbi, yenye namba za usajili MC 724 AKB ili apelekwe nyumbani kwake mtaa wa Mateka.

Wednesday 21 December 2016

Mapya yaibuka kaita sakata la Bwana harusi aliyemkimbia bibi harusi siku ya harusi Mbeya



Mapya  yameibuka sakata la kukwama kufungwa kwa ndoa ya Samwel Mwakalobo na Ginen Mgaya, baada ya kubainika kuwa moja ya sababu ni Bibi harusi mtarajiwa kuendeleza uhusiano na mzazi mwenzake.
Bwana harusi, Samuel Mwakalobo alitoweka muda mfupi kabla ya kufunga ndoa na Ginen Mgaya  katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Isanga jijini Mbeya.
Mwakalobo (26) alizua taharuki hiyo  Ijumaa ya Desemba 16, baada ya kutoonekana kanisani kufunga ndoa mbele ya Mchungaji Andagile Mwakijungu.
Habari zimedai kuwa kabla ya mpango wa kufunga ndoa hiyo, Mgaya tayari alishapata mtoto kabla hajaolewa, na Bwana harusi kubaini dakika za mwisho kuwa wawili hao walikuwa bado wana uhusiano wa karibu.

Monday 19 December 2016

MABAKI YA GOLIATI YAMEPATIKANA MAGHARIBI MWA JERUSALEMU


Kwa waliopitia Biblia kidogo bila shaka story ya Goliati,  jitu kubwa itakuwa si ngeni masikioni mwako.
Hivi karibuni huko Magharibi mwa Jerusalemu yamepatikana mabaki ya mifupa ya binadamu (skeleton ) yanayoaminika kuwa ni ya mtu wa zama hizo aliyefahamika kama Goliati ambaye aliuawa na Daudi kwa jiwe.
Mtaalamu ( archaeologist) Dkt.  Richard Martin kutoka Ujerumani amesema kwamba viashiria vilivyopo katika mabaki hayo yanaendana na story ya vita kati ya Daudi na Goliati iliyopo katika Biblia.
Kadhalika katika fuvu la kichwa katika mabaki hayo pamepatikana jiwe linalosadikika kupigwa na Daudi.

Sunday 18 December 2016

BWANA HARUSI AINGIA MITINI MUDA MCHACHE KABLA YA NDOA JIJINI MBEYA


Bibi harusi Given Mgaya Mkazi wa Isanga jijini Mbeya
Mwisho wa mwaka 2016 huenda ukamaliza na kituko cha aina yake katika  Mitaa ya Isanga Jijini Mbeya Mkoa wa Mbeya  mara baada ya bwanaharusi kuingia mitini masaa machache kabla ya kufunga ndoa.
Tukio hilo la aina yake limeibua maswali mengi kwa ndugu jamaa na marafiki ambao walikuwa tayari kwa maandalizi ya kuhudhuria harusi hiyo kuanzia kanisani hadi ukumbini.
Imeelezwa kuwa mipango yote ya harusi ilifanyika kwa pande zote mbili kushiriki kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa kufuatwa hadi hatua ya mwisho ya kuingia kanisani ambapo kama kawaida ndugu jamaa wote walihudhuria kanisani kwa lengo la kushuhudia  tukio hilo .
Tukio rasmi lilianza majira ya saa 7 mchana katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa   Isanga jijini Mbeya Desemba 16   ambapo kama kawaida Bibi harusi akiongozana na wapambe wake akifuata na msafara wa magari zaidi ya manne akitokea Saloon  na kuingia kanisani hapo.
Baada ya bibi harusi kuingia kanisani tayari kwa kufunga ndoa hiyo  taarifa zilianza kuenea kuwa bwanaharusi hayupo kanisani hapo na hajulikani mahali alipo.
Kadri muda ulivyozidi kwenda bila bwana harusi kufika kanisani hapo baadhi ya Ndugu, jamaa  na watu waliohudhuria harusi hiyo walianza kuhoji ambapo kwa muda huo yalipita zaidi ya masaa 4 bila chochote kuendelea kanisani hapo.

Akielezea mkasa huo Mchungaji kanisa la K.K.K.T Usharika wa Isanga Ndugu  Andagile Mwakijungu amesema jambo hilo amelipokea kwa masikitiko makubwa kwani halijawahi tokea toka ameanza kutoa  huduma kanisani hapo.
Amesema taratibu zote za kufungwa ndoa hiyo zilifanyika na Jana Desemba 15  majira ya saa 10 jioni  wahusika wote Samwel Mwakalobo   ambaye ni bwana harusi na Given Mgaya ambaye ni bibi harusi walifika nyumbani kwa baba mchungaji  na kuafikiana kuwa harusi hiyo ifanyike leo majira ya saa 7 mchana Desemba 16 kanisani hapo hivyo kitendo cha bwanahurusi kutofika bila sababu yoyote yeye mwenyewe imestua hasa kutokana na mipango ilivyokuwa imepangwa vizuri .
Amesema jambo hilo limetokea wakati yeye akiendelea kufanya maandalizi ya  kusubiri kutoa huduma ya kufunga ndoa kati ya wawili hao  .
Amesema wakati akiendelea kusubiri ili kufungisha ndoa hiyo walitokea ndugu upande wa mume ambao waliomba msaada kwa mchungaji ili awasaidie kumtafuta kijana wao ambaye ni bwanaharusi  kwa njia yoyote ili kufaham chanzo kilichopelekea kushindwa kufika kanisani hapo bila kutoa sababu zozote.
Amesema alichukua jukumu la kumtafuta kijana huyo ambapo alifanikiwa kumpata na kuzungumza nae ambapo kijana huyo alimueleza kuwa anatatizo na baadae angefika   kwa mchungaji ili kumueleza.

“Baada ya wazazi kufika na kunieleza kuwa nisaidie kumtafuta kijana wao nilichukua jukumu hilo na nilifanya hivyo na nilifanikiwa kumpata lakini alicho nijibu nikuwa mchungaji ninatatizo hivyo nitafika ofisini kwako kukueleza na kwa sasa nipo njiani nikitokea Tunduma ”Amesema
Mchungaji amesema kuwa wakati wanaendelea na majadiliano ya nini kifanyike  ghafla walipata ujumbe kutoka kwa mpambe wa bwanaharusi ambao ulitumwa na bwanahaurusi mwenyewe ukieleza  kuwa asingeweza kufika ili kufunga ndoa hiyo bila kueleza sababu yoyote.
Kufuatia tukio la bwanaharusi kuingia mitini huku jitihada za kumpata kushindiana Mchungaji huyo aliamua kusitisha zoezi la ufungaji wa ndoa hiyo.
“Nimejaribu kutafuta suluhisho la ndoa hii ili ifungwe licha ya kuchelewa lakini mpaka sasa hakuna dalili zozote kuwa ndoa hii itafungwa kwani bwanaharusi hajulikani alipo hivyo nimesitisha ndoa hii na niwaombee ndugu mkafanye jitihada zenu kumtafuta kijana huyu na mfikie muafaka kwa pande zote mbili ”Alisema Mchungaji.
Amesema taratibu za ndoa zinataka siku 21 ndoa ifungwe hivyo yeye kama mchungaji kisheria ndiye mdhamini na mtangazaji wa kisheria kwa suala la ndoa ya mwaka 71 ambayo inampa mamlaka ya kueleza kwanini ndoa haikufungwa  kwa siku 21 kwa mujibu wa sheria.
Bibi harusi atolewa kanisani akiwa amevuliwa shela …………………
Katika kile ambacho kilisubiliwa kwa hamu na ndugu na jamaa kuona hitimisho la ndoa hiyo  ambapo bibi harusi aliingizwa katika gari maalumu bila kuvalishwa shera pamoja na kufunikwa kanga na kuondoka kanisani hapo majira ya saa 10 jioni wakielekea pasipo julikana huku baadhi ya ndugu wakionesha majonzi na wengine kutokwa na machozi kwa kutoa amni kile kilichotokea .
Waliochanga kwa ajili ya sherehe ya usiku……………
Mara baada ya sinema hiyo kukamilika kanisani ndugu na jamaa waliochanga pesa zao kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya usiku walianza kueleza kuwa watafika ukumbini kama kawaida na kula chakula na kunywa ili kufidia pesa yao.
Sherehe hiyo ilipangwa kufanyika katika Ukumbi wa Mkapa Hall jijini Mbeya na kuhudhuriwa na watu zaidi ya mia tatu ambapokila kwa michango wanakamati ilikuwa laki moja na wengine shilingi elfu 70

Friday 16 December 2016

Utafiti wa NIMR Wagundua watu 83 waliougua ugonjwa wa zika Nchini



Watu 83 hapa chini wamegundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa zika kati ya watu 533 waliochukuliwa sampuli za damu hapa nchini Tanzania.
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini (NIMR) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki Bugando, umeonyesha kuwa watu hao walipata maambukizi hayo kati ya mwaka 2015 na mwaka 2016.
Wakati NIMR ikitoa ripoti yake ya utafiti kuhusu kugundulika watu waliokuwa na virusi vya zika nchini, Januari 31 Serikali ilitoa taarifa kukanusha kuwapo kwa ugonjwa huo nchini.
Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilitaarifu: “Kumekuwepo na taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya kitaifa na kimataifa kuhusu Homa ya Zika ambao ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi kijulikanacho kama “Zika Virus”.
“Ugonjwa wa Homa ya Zika bado haujaingia Tanzania. Wananchi waondoe hofu juu ya uwepo wa ugonjwa huu. Hata hivyo, ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya zika, dengue na malaria ambayo huenezwa kwa namna inayofanana.”

Aliyekuwa Mbunge wa kigoma kusini David Kafuulila Kuhamia Chadema



Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, (NCCR-Mageuzi) David Kafulila, amekihama chama hicho huku akieleza kuwa anajiandaa kuhamia Chadema.

Kafulila amethibitisha taarifa hizo na kusema tayari ameshawasilisha barua ya kujivua uanachama wa NCCR na kujiunga Chadema

“Nimewashukuru kwa kuwa pamoja katika kujenga chama na nafasi ya uenezi waliyonipa mara zote.
Nimeweka wazi kuwa natarajia kujiunga na Chadema. Nimeona kuwa kuna mahitaji ya watu wenye nia ya mabadiliko kuwa katika chama kimoja ili kufupisha safari.” alisema

Saturday 10 December 2016

Rais Dr John Pombe Magufuli afanya Mazungumzo na Dangote


Rais wa Jamhuri a Muungano wa Tanzania John Joseph Pombe Magufuli leo amekutana na Mmiliki wa Kiwanda saruji cha Dangote hii ni baada ya habari kutapakaa kuwa kiwanda hicho kimesitisha uzalishaji wa sariji kutokana kupanda kwa gharama za uzalisahji.

Monday 5 December 2016

Dangote kuja kushitaki kwa Magufuli



Sakata la kusimama kwa uzalishaji wa saruji katika kiwanda cha uzalishaji wa saruji cha Dangote mtwara laja na sura mpya baada ya mmiliki wa kiwanda hicho ALHAJ ALIKO DANGOTE kuamua kuja nchini kuonana na mkuu wan chi Mheshimiwa Dk John Pombe magufuli.
kwa taarifa tulizozipata mpaka sasa ni kwamba Mmiliki wa kiwanda hicho cha Dangote atakuja nchini kwa nia ya kuonana na Rais Magufuli ili kushtaki mambo kadhaa ikiwemo madai ya hujuma zinazofanywa na baadhi ya watu kwa sababu za kibiashara
kiwanda cha dangote ndio kiwanda kikubwa zaid afrika mashariki kwa uzalishaji wa saruji kilisitisha uzalishaji wa sarujiwiki kama mbili zilizopita kutokana na kile kilichoelezwa na Mkurugenzi Mtendaji mkuu wake Harpreet Duggal kuwa kiwanda kimeelemewa na gharama kubwa za uzalishaji

Mchezaji wa Mbao Fc U 20 afia uwanjani




Mshambuliaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 wa Mbao Fc Ismail Mrisho Khalifani alifariki dunia jana jion katika mechi kati ya timu yake na Mwadui Fc iliyokuwa ikipigwa katika uwanja wa kaitaba mjini Bukoba ikiwa ni mchezo wa mwisho wa kumaliza mzunguko wa kwanza.
Kifo cha mshambuliaji Khalfani kilitokea baada ya kugongana na beki wa Mwadui Fc wakati akiwania mpira , Khalifani alifanikiwa kuamka na kuanguka tena , kutokana nan a kukosekana na gari la huduma ya kwanza Khalifan alibebwa na gari la zima moto katika juhudi za kutaka kuokoa maisha ya marehemu lakini kabla hajafikishwa hosipitali alipoteza maisha.
Ismail Khalfan kabla umauti kumfikia katika mechi hiyo alifanikiwa kuipatia timu yake goli la pili kupitia adhabu ya mkwaju wa penati ambayo hadi mwisho wa mchezo Mbao Fc 2- 0 Mwadui Fc

Waziri Mkuu afanya ziara ya Kushtukiza katika hosptali ya Mout Meru Arusha


Waziri Mkuu majaliwa akiwafariji wazazi walioko katika wodi ya wazazi katika hosipital ya Mout Meru

Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana katika hali ya kushangaza alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya mkoa Mout Meru iliyoko mkoani Arusha. Ikumbukwe kuwa waziri mkuu yuko Arusha kwa ziara za kikazi.
Katika ziara hiyo ilitokana na malalamishi kutoka kwa wananchi juzi katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid kwamba hosipitali hiyo ina matukio ya wizi wa watoto wanaozliwa katika hospitali hyo.

Saturday 3 December 2016

Manyika apania kurejea katika kiwango chake Msimbazi



KIPA Manyika Peter wa Simba amesema anajifua ili kurudisha heshima yake kwenye kikosi cha Simba.
Akizungumza na mwandishiwetu wa habari jijin Dar es salaam, Manyika alisema kuwa ameamua kujifua asubuhi na mchana baada ya kuona anaweza kupoteza namb akabisa kwenye kikosi cha kwanza Simba.
“Mashabiki walianza kusema mimi kiwango changu kimeshuka, lakini sasa nimeamua kufanya mazoezi ili kurejesha heshima kwa mashabiki wangu,” alisema Manyika.
Pia Manyika alisema ataendelea kufanya mazoezi chini ya kocha Peter Manyika ambaye ni baba yake mzazi pia meneja wake hadi watakapoingia kambini. Manyika amekuwa kipa chaguo la pili kwa kocha mkuu wa samba na kuanzia msimu huu uanze hajacheza mchezo wowote wa Ligi Kuu Tanzania Bara.