Saturday, 3 December 2016

Manyika apania kurejea katika kiwango chake MsimbaziKIPA Manyika Peter wa Simba amesema anajifua ili kurudisha heshima yake kwenye kikosi cha Simba.
Akizungumza na mwandishiwetu wa habari jijin Dar es salaam, Manyika alisema kuwa ameamua kujifua asubuhi na mchana baada ya kuona anaweza kupoteza namb akabisa kwenye kikosi cha kwanza Simba.
“Mashabiki walianza kusema mimi kiwango changu kimeshuka, lakini sasa nimeamua kufanya mazoezi ili kurejesha heshima kwa mashabiki wangu,” alisema Manyika.
Pia Manyika alisema ataendelea kufanya mazoezi chini ya kocha Peter Manyika ambaye ni baba yake mzazi pia meneja wake hadi watakapoingia kambini. Manyika amekuwa kipa chaguo la pili kwa kocha mkuu wa samba na kuanzia msimu huu uanze hajacheza mchezo wowote wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Post a Comment