Rais wa Jamhuri a Muungano wa Tanzania John Joseph Pombe Magufuli leo amekutana na Mmiliki wa Kiwanda saruji cha Dangote hii ni baada ya habari kutapakaa kuwa kiwanda hicho kimesitisha uzalishaji wa sariji kutokana kupanda kwa gharama za uzalisahji.
Aidha katika mazungumzao hayo
Rais amemhakikishia mwekezaji hayo kwa serikali ya Tanzania itaelea kutengenza
mazingira mazuri kwa wawekezaji ili waweze Kufanya kazi vyema na kutimiza ndoto
ya Tanzania ya viwanda
Rais Magufuli amesema kuhusu
kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara hapakuwa na
tatizo lolote ila kulikuwa na watu ambao walitaka kujinufaisha binafsi kupitia
mradi huo kwa kufanya biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake
haikiruhusu. Amemtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni
chombo cha serikali badala ya kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza
faida tu. ''Iwapo unataka maelezo yoyote ama lolote linalokukwamisha uwasiliane
na viongozi wa serikali badala ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili ya
kufanya biashara ya ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili '' amesema Rais
Magufuli. Dokta Magufuli amesema Dangote ametaka eneo dogo ambalo angelitumia
kusafirishia saruji yake wakajitokeza watu ambao wametaka kumuuzia kwa shilingi
bilioni 43 kitu ambacho hakina uhalisia wowote bali ni watu ambao wanataka
kutengeneza faida kitu ambacho hakiwezekani. Kwa upande wake mmiliki wa Kiwanda
cha kuzalisha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote ameshangazwa na baadhi
ya vyombo vya habari kuwa amefunga kiwanda kwa sababu amekatazwa kuagiza makaa
ya mawe toka nje ya Tanzania kitu ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu
makaa ya mawe ya Tanzania ni rahisi na yana ubora kuliko kuagiza nje.
Katika kuthibitisha hilo, tayari
Mfanyabiashara huyo ameingiza malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji
yake. Ameongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza
faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo
hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini.
Alhaji Dangote amemuhakikishia Rais magufuli kuwa ataendelea kufanya kazi na
Serikali ya Tanzania na kamwe hana nia yoyote ya kufunga kiwanda chake kama
inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari bali ana mpango wa kuangalia fursa
nyingine zaidi za uwekezaji hapa nchini kutokana na uwepo wa sera nzuri za
uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.
No comments:
Post a Comment