Bibi harusi Given Mgaya Mkazi wa Isanga jijini Mbeya |
Tukio hilo la aina yake limeibua maswali mengi kwa ndugu
jamaa na marafiki ambao walikuwa tayari kwa maandalizi ya kuhudhuria
harusi hiyo kuanzia kanisani hadi ukumbini.
Imeelezwa kuwa mipango yote ya harusi ilifanyika kwa pande
zote mbili kushiriki kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa kufuatwa
hadi hatua ya mwisho ya kuingia kanisani ambapo kama kawaida ndugu jamaa
wote walihudhuria kanisani kwa lengo la kushuhudia tukio hilo .
Tukio rasmi lilianza majira ya saa 7 mchana katika kanisa
la K.K.K.T Usharika wa Isanga jijini Mbeya Desemba 16 ambapo kama
kawaida Bibi harusi akiongozana na wapambe wake akifuata na msafara wa
magari zaidi ya manne akitokea Saloon na kuingia kanisani hapo.
Baada ya bibi harusi kuingia kanisani tayari kwa kufunga
ndoa hiyo taarifa zilianza kuenea kuwa bwanaharusi hayupo kanisani hapo
na hajulikani mahali alipo.
Kadri muda ulivyozidi kwenda bila bwana harusi kufika
kanisani hapo baadhi ya Ndugu, jamaa na watu waliohudhuria harusi hiyo
walianza kuhoji ambapo kwa muda huo yalipita zaidi ya masaa 4 bila
chochote kuendelea kanisani hapo.
Akielezea mkasa huo Mchungaji kanisa la K.K.K.T Usharika wa
Isanga Ndugu Andagile Mwakijungu amesema jambo hilo amelipokea kwa
masikitiko makubwa kwani halijawahi tokea toka ameanza kutoa huduma
kanisani hapo.
Amesema taratibu zote za kufungwa ndoa hiyo zilifanyika na
Jana Desemba 15 majira ya saa 10 jioni wahusika wote Samwel Mwakalobo
ambaye ni bwana harusi na Given Mgaya ambaye ni bibi harusi walifika
nyumbani kwa baba mchungaji na kuafikiana kuwa harusi hiyo ifanyike leo
majira ya saa 7 mchana Desemba 16 kanisani hapo hivyo kitendo cha
bwanahurusi kutofika bila sababu yoyote yeye mwenyewe imestua hasa
kutokana na mipango ilivyokuwa imepangwa vizuri .
Amesema jambo hilo limetokea wakati yeye akiendelea kufanya
maandalizi ya kusubiri kutoa huduma ya kufunga ndoa kati ya wawili
hao .
Amesema wakati akiendelea kusubiri ili kufungisha ndoa hiyo
walitokea ndugu upande wa mume ambao waliomba msaada kwa mchungaji ili
awasaidie kumtafuta kijana wao ambaye ni bwanaharusi kwa njia yoyote
ili kufaham chanzo kilichopelekea kushindwa kufika kanisani hapo bila
kutoa sababu zozote.
Amesema alichukua jukumu la kumtafuta kijana huyo ambapo
alifanikiwa kumpata na kuzungumza nae ambapo kijana huyo alimueleza kuwa
anatatizo na baadae angefika kwa mchungaji ili kumueleza.
“Baada ya wazazi kufika na kunieleza kuwa nisaidie
kumtafuta kijana wao nilichukua jukumu hilo na nilifanya hivyo na
nilifanikiwa kumpata lakini alicho nijibu nikuwa mchungaji ninatatizo
hivyo nitafika ofisini kwako kukueleza na kwa sasa nipo njiani nikitokea
Tunduma ”Amesema
Mchungaji amesema kuwa wakati wanaendelea na majadiliano ya
nini kifanyike ghafla walipata ujumbe kutoka kwa mpambe wa bwanaharusi
ambao ulitumwa na bwanahaurusi mwenyewe ukieleza kuwa asingeweza
kufika ili kufunga ndoa hiyo bila kueleza sababu yoyote.
Kufuatia tukio la bwanaharusi kuingia mitini huku jitihada
za kumpata kushindiana Mchungaji huyo aliamua kusitisha zoezi la
ufungaji wa ndoa hiyo.
“Nimejaribu kutafuta suluhisho la ndoa hii ili ifungwe
licha ya kuchelewa lakini mpaka sasa hakuna dalili zozote kuwa ndoa hii
itafungwa kwani bwanaharusi hajulikani alipo hivyo nimesitisha ndoa hii
na niwaombee ndugu mkafanye jitihada zenu kumtafuta kijana huyu na
mfikie muafaka kwa pande zote mbili ”Alisema Mchungaji.
Amesema taratibu za ndoa zinataka siku 21 ndoa ifungwe
hivyo yeye kama mchungaji kisheria ndiye mdhamini na mtangazaji wa
kisheria kwa suala la ndoa ya mwaka 71 ambayo inampa mamlaka ya kueleza
kwanini ndoa haikufungwa kwa siku 21 kwa mujibu wa sheria.
Bibi harusi atolewa kanisani akiwa amevuliwa shela …………………
Katika kile ambacho kilisubiliwa kwa hamu na ndugu na jamaa
kuona hitimisho la ndoa hiyo ambapo bibi harusi aliingizwa katika gari
maalumu bila kuvalishwa shera pamoja na kufunikwa kanga na kuondoka
kanisani hapo majira ya saa 10 jioni wakielekea pasipo julikana huku
baadhi ya ndugu wakionesha majonzi na wengine kutokwa na machozi kwa
kutoa amni kile kilichotokea .
Waliochanga kwa ajili ya sherehe ya usiku……………
Mara baada ya sinema hiyo kukamilika kanisani ndugu na
jamaa waliochanga pesa zao kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya usiku
walianza kueleza kuwa watafika ukumbini kama kawaida na kula chakula na
kunywa ili kufidia pesa yao.
Sherehe hiyo ilipangwa kufanyika katika Ukumbi wa Mkapa
Hall jijini Mbeya na kuhudhuriwa na watu zaidi ya mia tatu ambapokila
kwa michango wanakamati ilikuwa laki moja na wengine shilingi elfu 70
No comments:
Post a Comment