Friday, 16 December 2016

Aliyekuwa Mbunge wa kigoma kusini David Kafuulila Kuhamia ChademaMbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, (NCCR-Mageuzi) David Kafulila, amekihama chama hicho huku akieleza kuwa anajiandaa kuhamia Chadema.

Kafulila amethibitisha taarifa hizo na kusema tayari ameshawasilisha barua ya kujivua uanachama wa NCCR na kujiunga Chadema

“Nimewashukuru kwa kuwa pamoja katika kujenga chama na nafasi ya uenezi waliyonipa mara zote.
Nimeweka wazi kuwa natarajia kujiunga na Chadema. Nimeona kuwa kuna mahitaji ya watu wenye nia ya mabadiliko kuwa katika chama kimoja ili kufupisha safari.” alisema
Post a Comment