Sakata la kusimama kwa uzalishaji wa saruji katika kiwanda
cha uzalishaji wa saruji cha Dangote mtwara laja na sura mpya baada ya mmiliki
wa kiwanda hicho ALHAJ ALIKO DANGOTE kuamua kuja nchini kuonana na mkuu wan chi
Mheshimiwa Dk John Pombe magufuli.
kwa taarifa tulizozipata mpaka sasa ni kwamba Mmiliki wa
kiwanda hicho cha Dangote atakuja nchini kwa nia ya kuonana na Rais Magufuli
ili kushtaki mambo kadhaa ikiwemo madai ya hujuma zinazofanywa na baadhi ya
watu kwa sababu za kibiashara
kiwanda cha dangote ndio kiwanda kikubwa zaid afrika
mashariki kwa uzalishaji wa saruji kilisitisha uzalishaji wa sarujiwiki kama
mbili zilizopita kutokana na kile kilichoelezwa na Mkurugenzi Mtendaji mkuu wake
Harpreet Duggal kuwa kiwanda kimeelemewa na gharama kubwa za uzalishaji
Kwa upande mwingine mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini,
Esther Baruti alitudokeza jana jion kuwa
boss wake ameamua kupanga ziara ya kuja nchini kuzungumza na Rais Magufuli juu
ya vikwazo vinavyoukabili mradi huo wa dangote wa uzalishaji wa saruji ulio na
dhamni ya zaid ya paundi million 500 za kimarekani
Aliendelea kueleza kuwa kuna mambo mengi tuliyokubaliana na
serikali kabla ya kuamua kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa na hakuna tatizo na
serikali maana imetupa msamaha wa kwenye kodi kwenye mambo mengi kuanzia kwenye
mambo kama ardhi, mafuta ya dizeli lita million miatatu na mambo mengine mengi
tu.
No comments:
Post a Comment