
(Independent), vipimo vya afya vya Di Maria vimechelewa kwa sababu alikuwa amechoka baada ya kusafiri kwa saa 20 akitokea Agrentina kwenda Doha (Daily Mail), Manchester United watamsajili Pedro kutoka Barcelona kwa pauni milioni 20 katika saa 48 zijazo, na huenda pia wakamchukua beki wa kati wa Real Madrid, Pepe (Daily Mirror), Southampton wametoa dau la pauni milioni 7 kumtaka beki wa kati wa Celtic Virgil van Dijk, 24 ambaye pia amehusishwa kwenda Arsenal na Manchester United (Daily Express), Sunderland wanakaribia kukamilisha uhamisho wa mkopo wa viungo Yaan M'Villa na Leroy Fer kutoka Rubin Kazan na QPR (Shields Gazette), winga wa Barcelona Adama Traore, 19 anasafiri kwenda Liverpool wakati akijiandaa kuijiunga na klabu hiyo ingawa amehusishwa na kwenda Bayern Munich, Manchester City, Manchester United na Sevilla (Sport), Christian Benteke amepewa jezi namba 9 ya Liverpool, ambayo iliwahi kuvaliwa na Ian Rush na Robbie Fowler (Daily Express), Manchester United wamemwambia kipa Andres Lindegaard kuwa anaweza kuondoka (Daily Mail), Newcastle United wameongeza kasi yao ya kutaka kumsajili Jesse Lingard wa Manchester United (ESPN), meneja wa Lyon, Hubert Fournier amemwambia mshambuliaji Alexandre Lacazette anaweza kuondoka kama hana furaha ya kuichezea klabu hiyo (L'Equipe), Arsenal nao wamejiunga katika mbio za kutaka kumsajili Denis Cheryshev wa Real Madrid (AS), Manchester City wanamnyatia Isco wa Real Madrid (Sport), Juventus wamekataliwa dau lao na Barcelona la kumtaka Javier Mascherano, ingawa mchezaji mwenyewe anataka kuhamia Italia (Tuttosport), Manchester City wameambiwa wanaweza kuanza mazungumzo juu ya Kevin de Bruyne wa Wolfsburg lakini waanzie na dola milioni 78 (Daily Mail)
No comments:
Post a Comment