Mwenyekiti
wa chama cha wananchi CUF Prof Ibrahimu Haruna Lipumba amejiuzulu
nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho kikongwe hapa nchini.
Baada ya minongono ya kutaka kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti kwa
kile kilichodaiwa ni maelewano hasi na baadhi ya wakurugenzi wa chama
hicho sasa ni rasmi.
Prof Lipumba aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza kushika nafasi hiyo
mwaka 1999 kuhusu mchakato wa katiba amesema kwa sasa haoni kama UKAWA
utafanikisha upatikanaji wa katiba bora itakayoweza kukidhi tunu za
taifa, utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi na uwajibikaji, msomi huyo
wa mashuhuri wa masuala ya uchumi nchini amesema katika kipindi hiki
kabla ya uchaguzi atajikita zaidi katika kuandaa ushauri wa mambo
mbalimbali yanayopaswa kutekelezwa na serikali ijayo ambapo baada ya
uchaguzi atajikita katika masuala ya kitafiti pekee.
Bw Jusa Ismail ni naibu katibu mkuu wa CUF Tanzania Zanzibar ambapo
anakiri ofisi ya katibu mkuu kupokea taarifa za kujiuzulu mwenyekiti wa
chama hicho makao makuu ya chama hicho Buguruni Dar es Salaam wanachama
wa CUF walikuwa na mitazamo tofauti kuhusu taarifa hiyo ya kujiuzulu
mwenyekiti wao.
Prof Ibarhimu Lipumba ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo jijini Dar
es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari ambao hata hivyo
haukuhusisha kiongozi yeyote wa chama cha wananchi CUF.
No comments:
Post a Comment