Saturday 15 August 2015

Viongozi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro wajiunga Chadema.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) na katibu wa fedha na uchumi wa chama cha mapinduzi(CCM) wa mkoa wa Kilimanjaro wamejiuzulu uongozi wa chama hicho na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo( Chadema).
Wakizungumza na waandishi wa habari mjini moshi viongozi hao ambao ni mwenyekiti wa umoja wa vijana(UVCCM)mkoa wa Kilimanjaro Bw.Fredrick Mushi na katibu wa fedha na uchumi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro Bw.Paul Matemu wamesema wamechoshwa na mwendo wa chama hicho.
 
Akijibu tuhuma za jeshi la polisi za kuzuia msafara wa waziri mkuu mstaaafu Mh.Edward Lowassa kuhudhuria mazishi ya muasisi wa chama cha mapinduzi marehemu Peter Kisumo kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Bw.Fulgence Ngonyani amekanusha taarifa za jeshi la polisi kumzuia waziri mkuu huyo mstaafu Mh.Edward Lowassa na kusema kwamba walizuia msafara wa vyama vinavyounda UKAWA kutokana na msafara huo kuwa na idadi kubwa ya pikipiki na magari.

No comments: