Monday 10 August 2015

Zaidi ya wanachama 100 wa CCM warejesha kadi na kujiunga na Chadema Bukoba.

Zaidi ya wanachama miamoja akiwemo mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Bukoba jimbo la Bukoba mjini ambae pia ni diwani wa kata ya kahororo Chief Kalumuna wamerejesha kadi za chama cha mapinduzi na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo Chadema.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Bukoba mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor Sherejei amesema wanachama hao ambao wengiwao wamepelekea kadi hizo kimyakimya kwa muda wa siku saba na kufikia wanachama miamoja hamsini wameamua kufanya hivyo kwaajili ya kumuunga mkono waziri mkuu mstaafu Edward Ngoyai Lowassa na kuhakikisha anapata kiti urasi amwamu ya tano kupitia chama hicho. 
 
Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapindi jimbo la Bukoba mjini ambae pia ni diwani anae maliza mudawake katika kata ya Kahororo Chiefu Kalumuna amesema yeye amekuwa mpinzani ndani ya chama kwa kipindi kilefu na sasa ameamua kukihama chama chake kutokana na uonevu pamoja na mabavu yanayotumiwa na viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho kwakukata majina ya wanachama wanokuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wananchi ili wasigombee nafasi mbalimbali za uongozi hatakama wanakulika na wananchi.

No comments: