Maelfu
ya wananchi wa ndani na nje ya mkoa wa Arusha wamejitokeza kumpokea na
kumsikiliza mgombea urais wa CHADEMA kupitia UKAWA na waziri mkuu wa
zamani Mh. Edward Lowasa huku wakishuhudu wanachama wa (CCM) na
viongozi akiwemo aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani Mh.Laurence
Masha.
Wengine waliojiunga na CHADEMA ni pamoja na katibu wa CCM wa wilaya
ya babati Bw,Daniel Porokwa,Mwenyekiti wa UWT,wa wilaya ya karatu bi
fabiola manimo katibu wa UWT wa wilaya ya Siha,na aliyekuwa mwenyekiti
wa CCM wa mkoa wa Arusha kwa zaidi ya miaka 20 Mh.Yona Nnko.
Pia naye Mwenyekiti wa vijana wa CCM mkoa wa Arusha Bw.Robson
Naitinyiku,aliyegombea Ubunge wa jimbo la Simanjiro na kushika nafasi ya
pili Bw.Lenana Lenganasa,Diwani wa kata ya Ruvu Remiti wilayani
Simaniro Bw,Siyoi Solomoni sumari na kiongozi mkuu wa ukoo wa ukoo wa
nanyaro kutoka Arumeru Mashariki.
Baada ya kazi ya kuwapokea wanachama wapya kukamilika viongozi wa
ngazi mbalimbali wa UKAWA akiwemo muasisi wa CHADEMA Mzee Edwin Mtey
wakatoa salam huku wakiendelea kuwataka watanzania kupokea mabadiliko
na kuhakikisha kuwa yanafanyika kwa amani.
Ukafika wakati wa mgombea urais wa CHADEMA kupitia umoja wa UKAWA
Mh.Edward Lowasana mgombea Mwenza Mh.Duni Haji ambao wameendelea
kuwataka wananchi kudumisha umoja na ushirikiano ili waweze kushinda
uchaguzi na kupata nafasi ya kukabiliana na matatizo mbalimbali
yanayowakabli wananchi.
No comments:
Post a Comment