Ni tambo za ushindi za Edward Lowasa alizozitoa dakika chache baada
ya kupitishwa na mkutano mkuu wa Chadema kuwa mgombea pekee wa nafasi
ya urais kwa tiketi ya Ukawa na kuvunja minongon iliyokuwa imetanda kuwa
Ukawa isingefikia hatua hiyo.
Katika hutuba yake kwa wajumbe wa mkutano mkuu Lowasa amesema
anaamini kwa ushirika imara wa Ukawa wataweza kushinda viti vingi vya
ubunge na nafasi ya urais huku akijinasibisha kuwa nguvu, nia na uweza
wa kufanisha ushindi wa zaidi ya silimia 80 kwa nafasi ya urais.
Kwa muda mrefu amekuwa akinyoshewa kidole kuwa huenda akavunja
muungano endapo atafanikiwa kuwa rais wa Zanzibar, lakini anasema
muungano wa Tanzania utakuwa imara zaidi chini ya uongozi wa serikali ya
Ukawa.
Awali akifungua mkutano mkuu wa Chadema mwenyekiti wa chama hicho
Freeman Mbowe amewataka watanzania kujiandaa kisaikolojia kwani ni
dhahili sasa safari ya uhakika imewadia.
James Mbatia ni moja ya viongozi wa Ukawa ambapo amevitaka vyombo
vya ulinzi nchini kuhakikisha haviegemei upande wowote hasa katika
kipindi cha uchaguzi mkuu, mkutano mkuu wa Chadema uliofanyika jijini
Dar es Salaam na kuhudhulia na viongozi mbalili wa ndani na nje ya nchi
pia umewapokea na kuwakabidhi kadi baadhi ya vigogo wa CCM wakiongozwa
na mwenyekiti wa wenyeviti wa miko ya CCM Bw Mgana Msindai.
No comments:
Post a Comment