Maafisa
wa Polisi nchini Israeli wamesema kuwa wamewakamata watu 7
wanaoshukiwa kwa kuvamia nyumba moja ya mpalestina katika ukingo wa
magharibi na kuiteketeza moto.
Shambulizi hilo lililotokea mwisho wa mwezi uliopita lilisababisha kifo cha mtoto wa mwaka mmoja u nusu.Shambulizi hilo lililotekelezwa na walowezi wa Kiyahudi lilimuacha bwana Dawabsheh mke wake na mwana wao mwenye umri wa miaka 4 wakiuguza majereha mabaya.
Sa'ad Dawabsheh aliaga dunia katika hospitali ya Soroka iliyoko Israeli alikokuwa akipokea matibabu baada ya kuungua sehemu kubwa ya mwili wake.
Mke wake bi Riham na mwana wao wa kiume Ahmad bado wako katika hali mahututi hospitalini.
Kulingana na ripoti hiyo ya Polisi washukiwa hao walikamatwa katika operesheni iliyofanywa katika makao haramu ya walowezi katika ukingo wa Magharibi.
No comments:
Post a Comment