Gari la Mh Lowassa ambaye pia ni mgombea urais wa Chadema
akiwakilisha Ukawa lilianza kufuatwa na magari mengine ya watu binafsi
na pikipiki baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro
akitokea na Dar es Salaam na alipofika Moshi kundi la vijana walifunga
barabara na kulazimika kuingia katika hotel ya kizi ambako pia
walimfuata na kuzingira lango kuu na licha ya kuwasihi kuwa wampe nafasi
aende kwenye mazishi vijana hao waliendelea kulifuata gara lake.
Katika hali ambayo sio rahisi kuamini vijana hao wakiwa na pikipiki
waliendelea kufuata gari la Mh Lowassa hadi Mwanga na alipoanza safari
ya kuelekea Usangi takrbani kilometa moja kutoka barabara kuu polisi
wakafunga barabara hali iliyosababisha mvutano mkubwa na jambo ambalo
limelalamikiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya viongozi akiwemo
mwenyekiti wa NCCR mageuzi James Mbatia na Mh Agustino Mrema.
Baada ya vuta nikuvute kati ya polisi na wananchi na viongozi hao
wa vyama vya siasa mkuu wa polisi wa wilaya ya Mwanga aliruhusu watu
waliokuwa na pikipiki kuendelea na safari kwa masharti ya kuondoa
bendera za vyama vyao na pia kwenda bila msafara maelekezo ambayo licha
ya kubalika utekelezaji wake ulikuwa mgumu na kusababisha kuendelea kwa
malumbano na ndipo Mh Mbatia akata taarifa za Mh Lowassa kusitisha
safari na kuamua kurudi Moshi na hatimaye Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment