Wednesday, 21 May 2014

Moubarak Jela Miaka Mitatu kwa Ufisadi

Hosni Moubarak katika chumba cha watuhumiwa ambacho kilizunguushwa kwa vyuma,katika kesi inayomkabili, arili 15 mwaka 2013 mjini Cairo.
Hosni Moubarak katika chumba cha watuhumiwa ambacho kilizunguushwa kwa vyuma,katika kesi inayomkabili, arili 15 mwaka 2013 mjini Cairo.
Rais wa zamani wa Misri Hosni Moubarak amehukumiwa leo jumatatu miaka mitatu jela, baada ya kupatikana na kosa la kashfa ya ufisadi wa mali ya umma. Hukumu hii inakuja baada ya miaka mitatu na nusu kutimuliwa kwenye uongozi wa nchi kufuatia maandamano ya raia, baada ya kuwa katika utawala kwa muda wa miaka 30.

Moubarak, mwenye umri wa miaka 86, alisikilizwa kipindi kirefu mahakamani kuhusu tuhuma hizo zinazomkabili. Moubarak amekua amekaa leo jumatanu kwenye kiti cha magurudumu, akiwa karibu ya watuhumiwa wenzake ndani ya chumba kiliyozunguushwa vyuma.
Wanae Gamal pamoja na Alaa wamehukumiwa kifungo cha miaka minne jela, wakiwa katika kesi moja na baba yao, huku watuhumiwa wengine wakiwa wameachiwa huru
Rais huyo wa zamani wa Misri, alihukumiwa mara ya kwanza katika mahakama ya Cairo baada ya kupatikana na kosa la kashfa ya rushwa, akituhumiwa kupitisha mlango wanyuma zaidi ya milioni 100 pesa za Mirsi sawa na (Uro milioni 10), ambazo zilikua zilitengwa kwa bajeti ya ikulu.
Alihukumiwa pia katika kesi ihusuyo vifo vya waandamanaji wakati wa maandamano yaliyompelekea kung'olewa madarakani mwanzoni mwa mwaka 2011.
Kufuatia kesi hio alihukumiwa mara ya kwanza mwaka 2012 kifungo cha maisha jela, kabla ya mahakama ya juu kuamuru kesi hio irejelewe kusikilizwa.
Hukumu hii inatolewa zikisaliya siku 5 tu ili kufanyike uchaguzi wa urais, ambao unampa nafasi kubwa ya ushindi kiongozi wa zamani wa kijeshi, abdel Fattah al-Sissi, ambae alimtimua madarakani rais Mohamed Morsi, ambae alihukumiwa hivi karibuni kifungo cha maisha jela.

No comments: