Tuesday 13 May 2014

Msako wa Polisi dhidi ya washukiwa wapelekea mashaka katika baadhi ya makanisa Kenya.


Vijana karibu na Msikiti wa Musa Mombasa wakilalamika dhidi ya uvamizi wa polisi.
Vijana karibu na Msikiti wa Musa Mombasa wakilalamika dhidi ya uvamizi wa polisi.
Ukamataji  wa serikali dhidi ya wanamgambo wakiislam huenda umekuwa na athari zisizotegemewa kwa baadhi ya makanisa nchini Kenya. Kwa muda wa miaka miwili iliyopita, kanisa la Salvation Army limekuwa  lengo la  mashambulizi yanayofanywa na vijana wa kiislamu, waliokasirishwa  na kile  wanachofikiria  ni ukamataji  mbaya unaofanywa na polisi dhidi ya  washukiwa wanamgambo.
Kanisa la salvation Army  lipo katika  eneo la  majengo mjini Mombasa tangu mwishoni mwa miaka ya 1920. Katika miaka ya karibuni, kanisa hilo limekuwa likishambuliwa na vijana wa kiislamu ambao wamekuwa wakipambana na polisi kupinga vifo vya viongozi wa dini na vijana, katika ukamataji  wa serikali dhidi ya wanamgambo wa Al Shabab.
Uharibifu unaonekana bayana  kutokana na shambulizi la mwezi October, pale washambuliaji walipo rusha mabomu ya petroli kwenye kanisa hilo, na kuchoma ukumbi wa mafunzo na chumba cha kuhifadhia vitu.
Miezi sita baadae, wasi wasi wa usalama  umepelekea  maafisa wawili wa polisi kupelekwa kuwalinda zaidi ya waumini  100 kila jumapili.Lakini licha ya vitisho, Mary Ivusa mwenye umri wa miaka 51, bado anafika kanisani lakini ana wasiwasi juu ya kutokea kwa mashambulizi mapya.
Anasema “Khofu, khofu ni kubwa sana katika  maisha yetu kwa sababu kama kina mama, tunakuja na watoto wetu wadogo ambao hawawezi kukimbia, ambao bado ni wadogo, kwa hivyo  ni khofu iliyo katika maisha yetu. Na hilo ndiyo linalotufanya kuwa na khofu, pale inapokuwa hakuna usalama wa kutosha.”

Mwezi Aprili, wanaume wawili waliokuwa na bunduki, waliingia katika kanisa moja kwenye eneo la Likoni mjini Mombasa, na kufyatua risasi, na kuua waumini 4, na kuwajeruhi wengine 15.
Ivusa ambaye ni mama wa watoto watatu, anasema shambulizi hilo limewafanya watu wengi kukhofia kuja kanisani.
Tangu kutokea kwa shambulizi hilo, serikali imeweka  huduma za usalama kwenye  makanisa, haswa katika miji ya pwani. Wachambuzi wa usalama wa kieneo, wanasema  baadhi ya vijana wa kiislamu wanaelekeza hasira zao kwenye makanisa kwa sababu ya kupotea  na kuuwawa kwa viongozi wakiislamu na vijana wanaoshutumiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al shabab nchini  Somalia.
Taasisi za ndani za haki za binadamu zinawashutumu polisi wa kenya  kwa  kutumia nguvu kubwa  dhidi ya jamii za kiislamu, ikiwa ni pamoja na kuwatokomeza kwa nguvu au mauaji.  Polisi wanakana tuhuma hizo na kusema wanalitetea taifa kutokana na mashambulizi.
Sergent Meja  Alfred  Charles Mugo , mzee  katika kanisa la Salvation army Mombasa, anasema  wakristo hawajawakosea  vijana wa kiislamu, na kwamba wanapaswa kutumia njia sahihi kuelezea malalamiko yao.

No comments: