Serikali halali iliyochaguliwa na
wananchi wa Palestina inayoongozwa na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu
wa Palestina HAMAS imesema kuwa, kurejeshwa wakimbizi wa Kipalestina
kwenye ardhi zao za asili ni mstari mwekundu na suala hilo halihitajii
mazungumzo ya aina yoyote. Muhammad al Mad houn Waziri wa Vijana,
Michezo na Utamaduni wa serikali halali ya Palestina ameyasema
hayoUkanda wa Ghaza wakati wa kuadhimisha kutimia miaka 66 ya kukaliwa
kwa mabavu ardhi za Palestina na kuongeza kuwa, wananchi wa Palestina
kamwe hawatafumbia macho hata chembe haki zao na wataendelea kufanya
juhudi za kuhakikishakwamba kadhia ya wakimbizi wa Kipalestina inakuwa
ya kimataifa. Waziri Mad houn ameongeza kuwa, serikali yoyote
itakayokuja madarakani inapasa kufungamana kikamilifu na haki zote za
wananchi wa Palestina. Hivi sasa kuna Wapalestina zaidi ya milioni tano
na nusu waliolazimika kuwa wakimbizi kutokana na hatua ya utawala wa
Israel kuzikalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina. Inafaa kuashiria hapa
kuwa utawala ghasibu na bandia wa Israel ulitangazwa kuwepo kwake tarehe
14 Mei 1948 kwa uungaji mkono wa Uingereza.
No comments:
Post a Comment