“Huwezi kusimama hapa mtu na macho yakakutoka halafu unaanza kulizungumzia taifa lingine ambalo siyo lako, hivi unatoa wapi ujasiri huo au wanakulipa,”alihoji Membe na kuongeza
Wakati Bunge likipitisha bajeti ya makadirio ya matumizi Sh191.91 bilioni ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2014/15 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alitumia nafasi hiyo ‘kumchana’ Ezekiel Wenje na kusema kuwa anatumiwa na mataifa ya nje.
Mbali na hivyo aliwaita watu wanaotoa kauli za
uchonganishi kuwa ni wapumbavu na akataka waache tabia za kipumbavu
kwani hawatavumiliwa hata kidogo.
Membe alitoa kauli hiyo jana jioni wakati akitoa
majumuisho katika michango ya wabunge kwenye hotuba ya mapato na
makadirio ya wizara hiyo kwa mwaka 2014/15.
Wenje ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jana asubuhi katika hotuba yake,
alimshambulia Membe kuwa ni waziri mzigo ambaye hajui wajibu wake.
Sakata hilo liliibuliwa kwenye uhusiano baina ya Tanzania na nchi ya Rwanda ambalo Wenje alilizungumzia zaidi.
Akijibu hoja hizo Membe, alisema: “Kwanza
nikubaliane na kauli ya wabunge wengi kuwa uhusiano wa Tanzania na
Rwanda siyo mzuri kwani kila upande haumuamini mwenzake,” aliema Membe.
Alisema kinachowaumiza pande zote ni kuwa kila
upande unapozungumza na mahasimu wa mwenzake, wanahisi kuwa anataka
kuipindua Serikali yao hivyo bado hawajakubaliana kwa jambo lolote
lakini akasema yote yatakwisha salama.
“Huwezi kusimama hapa mtu na macho yakakutoka
halafu unaanza kulizungumzia taifa lingine ambalo siyo lako, hivi unatoa
wapi ujasiri huo au wanakulipa,”alihoji Membe na kuongeza.
“..Mimi naweka rehani uwaziri wangu hapa kwamba
ukileta vielelezo kamili mimi nitakuwa tayari kuachia nafasi yangu, je
na wewe nikitoa vielelezo utakuwa tayari kuwajibika.”
Alimtaja Wenje kwa jina kuwa alichokifanya hakifai
kuwa alitoa kauli ambayo siyo nzuri kwa siri za taifa na akasema mtu
kama huyo akipata nafasi hata kama nchi itakuwa vitani, yuko tayari
kutoa siri.
Aliyataja makundi ya ya M23 kuwa ni moja ya kundi
ambalo linaundwa na Banyamulenge waliokuwa chini ya Roral Nkunda pamoja
na kundi la FDRA ambalo liliua watu wengi kwamba linaundwa na Wahutu
bila ya ubishi.
Membe alimpongeza mbunge Alli Keissy kuwa
alichokizungumza jana asubuhi kuhusu Rwanda na DRC Kongo ni sahihi na
ndiyo maana alimshangilia kwa nguvu zote.
No comments:
Post a Comment