Baraza la Usalama |
Suala la waasi wa LRA walioko kwenye maeneo ya Afrika ya Kati limemulikwa leo katika Baraza la Usalama, huku Baraza hilo likisikiliza ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu Ofisi ya Umoja wa Mataifa katika eneo hilo, UNOCA. Grace Kaneiya na taarifa kamili.Ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu eleo la Afrika ya Kati imewasilishwa na Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu katika eneo hilo anayeondoka, Abou Moussa, ambaye amesema ziara zake hivi karibuni nchini Chad, Cameroon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, zilidhihirisha athari za mzozo wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa ukanda mzima, zikiwemo changamoto za kibinadamu dhidi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali za kikanda.
"Mataifa haya pia yalielezea wasiwasi wao kuwa usambazaji
wa silaha, vitendo vya makundi yenye silaha na ghasia za kidini huenda
zikaenea na kuvuka mipaka na hivyo kutatiza utulivu katika nchi zao"
Bwana Mousa amesema ofisi ya UNOCA inaendelea kushirikiana
Muungano wa Afrika, kuratibu juhudi za kimataifa chini ya utaratibu wa
kikanda wa Umoja wa Mataifa kukabiliana na tishio na madhara ya waasi wa
LRA.
"Nafurrahia kulieleza Baraza hili kuwa idadi ya vifo vitokanavyo na
LRA, watu wanaotekwa na wanaolazimika kuhama makwao imeendelea kupungua,
huku hatua za kijeshi na kampeni ya kuwashawishi wafuasi kujisalimisha
zikiwa zimeidhoofisha LRA zaidi."
No comments:
Post a Comment