Friday, 30 May 2014
Boko haramu wateka viongozi wawili
Watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa ni kutoka kundi
la Kiislamu la Boko Haram wamewateka nyara viongozi
wawili wa kikabila wa Kiislamu kaskazini mashariki ya
Nigeria leo. Watu hao wenye silaha wamewateka
mtawala wa eneo la Gwoza, Alhaj Idriss Timta , na
mtawala wa Uba, Alhaj Ismaila Mamza, waliokuwa katika
magari yao katika mji wa Zhur, eneo la ndani katika
eneo la kusini mwa jimbo la Borno. Duru za kiusalama
na afisa wa jimbo la Borno ameliambia shirika la
habari la Reuters kuwa watu hao walikuwa wakielekea
katika mazishi. Duru moja ilisema kuwa jeshi limewekwa
katika eneo hilo kuwatafuta mateka , licha ya kuwa
ujumbe kama huo kila mara huambatana na hatari
kubwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment