Katika baraza hilo la mawaziri linalojumuisha
wabunge wanaotokana na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), mawaziri 25
wanatoka Chadema, 11 wanatoka CUF na NCCR-Mageuzi ni wanne.
Mawaziri kivuli walioachwa katika baraza hilo ni
Sylvester Kasulumbay (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), Highness Kiwia
(Viwanda na Biashara) na Rose Kamili (Kilimo, Chakula na Ushirika).
Wengine walioachwa na Mbowe akasisitiza kuachwa
kwao siyo kwa sababu hawawezi kazi bali ni kutaka kuwa na baraza la
mawaziri dogo ni Sabrina Sunga (Naibu Waziri Maji).
Katika Baraza hilo, nafasi ya mnadhimu mkuu wa
upinzani Bungeni iliyokuwa ikishikiliwa na Tundu Lissu (Chadema) sasa
itashikiliwa na Mbunge wa Tumbe, Rashid Abdalah kutoka chama cha CUF.
Akitangaza baraza hilo Bungeni mjini Dodoma jana,
Mbowe alisema Wizara ya Katiba na Sheria imeongezewa majukumu ya
Muungano na waziri wake atakuwa ni Lissu na naibu wake ni Abdalah.
Pia amemteua Mbunge wa kuteuliwa na Rais ambaye
pia ni Mwenyekiti wa taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ambaye anakuwa
Waziri wa Fedha wakati Naibu wake atakuwa Christina Lissu kutoka
Chadema.
Mawaziri Ofisi ya Rais ni Profesa Kulikoyela
Kahigi (Utawala Bora-Chadema), Vicent Nyerere (Utumishi-Chadema) na
Esther Matiko (Mahusiano na Uratibu-Chadema).
Ofisi ya makamu wa Rais itakuwa na mawaziri wawili
ambao ni mchungaji Israel Natse kutoka Chadema atakayeshughulika na
Mazingira na Naibu wake atakuwa ni Assah Othman Hamad (CUF).
Mnadhimu wa Upinzani Bungeni ndiye atakayeshikilia pia nafasi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mazingira.
Mawaziri katika ofisi ya Waziri mkuu ni Pauline
Gekul (Uwekezaji na Uwezeshaji-Chadema), Rajabu Mohamed Mbaruku (Sera,
Uratibu na Bunge-CUF) na David Silinde (Tamisemi-Chadema).
Wizara ya Chakula, Kilimo na Ushirika itashikiliwa
na Meshack Opulukwa (Chadema), Wizara ya Nishati na Madini atakuwa John
Mnyika Chadema na Naibu wake “atakuwa Raya Ibrahim (Chadema).
Kulingana na orodha hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa itashikiliwa na Ezekiah Wenje (Chadema) na Naibu wake ni
Rashid Abdalah kutoka CUF.
Mawaziri wengine na wizara zao kwenye mabano ni
Felix Mkosamali (Ujenzi-NCCR-Mageuzi), Magdalena Sakaya (Maji-Cuf), na
Moses Machali (Uchukuzi- NCCR- Mageuzi).
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itaongozwa na
Godbless Lema wa Chadema na Naibu wake ni Khatibu Said Haji wa CUF
wakati Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi ni Halima Mdee wa Chadema.
Kwa mujibu wa orodha hiyo, Mbowe amemteua Rose
Kamili Sukum kutoka Chadema kuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
wakati Naibu wake atakuwa ni Mkiwa Adam Kiwanga wa CUF.
Wizara ya Maliasili na Utalii itashikiliwa na
mchungaji Peter Msigwa (Chadema), Wizara ya Ushirikiano wa Afrika
Mashariki imeenda kwa Joseph Selasini (Chadema) na naibu ni Rukia Ahmed
Kassim (CUF).
Mbowe pia amemteua Masoud Abdalah Salim wa CUF
kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na Wizara ya Elimu
itashikiliwa na Susan Lyimo na Naibu wake ni Joshua Nasari wote toka
Chadema.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeenda kwa Dk
Gervas Mbassa na Naibu wake ni Conchesta Rwamlaza wote wa Chadema. David
Kafulila (NCCR) ameteuliwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
Katika baraza hilo la mawaziri, Injinia Habib
Mnyaa wa CUF ameteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia wakati Lucy Owenya kutoka Chadema akiteuliwa kuwa naibu wake.
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto imeenda kwa
Baruan Salum Khalfan wa CUF na Naibu wake ni Subreena Sungura wa
Chadema. Cecilia Paresso wa Chadema anakuwa Waziri wa Kazi na Ajira.
Wizara ya Habari, Vijana na Michezo imeendelea kushikiliwa na Joseph Mbilinyi wa Chadema.
Akizungumza na wanahabari, Mbowe alisema wakati
katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya CCM, wanaume ni 36 na wanawake
15, wao upinzani wanaume ni 26 na wanawake ni 14.
Hali kadhalika Mbowe alisema wakati Baraza zima la
mawaziri la Serikali ya CCM likiwa na mawaziri kamili 28 na manaibu 22,
wao Baraza lao Kivuli lina mawaziri kamili 28 na naibu mawaziri 12.
Alisema nafasi ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Ubungeni iliyokuwa ikishikiliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe itantangazwa baadaye
Alisema nafasi ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Ubungeni iliyokuwa ikishikiliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe itantangazwa baadaye
Habari hii imeandikwa na Daniel Mjema, Sharon Sauwa na Fidelis Butahe
No comments:
Post a Comment