Watu 15 wamefariki katika mkanyagano uliozuka uwanjani katika Jamhuri ya Congo
Katika mechi kati ya klabu ya AS Vita na Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Congo, watu 15 walipoteza maisha yao baada ua kuzuka kwa mkanyagano.
Stesheni ya redio ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Okapi ilitaarifu kuwa kutokana na duru kutoka Wizara ya Maswala ya Ndani, watu 15 walifariki na 20 kujeruhiwa baada ya mkanyagano kuzuka katika mechi hiyo ambapo Tout Puissant Mazembe walikuwa wenyeji wa wapinzani wao AS Vita.
Kulingana na taarifa kutoka tovuti ya mtandao ya timu hiyo ya TP Mazembe iliyoibuka mshindi wa 1-0, vurugu hiyo ilizuka baada ya polisi waliogadhabishwa kurusha vitoa machozi kwa upande wa wapinzani AS Vita.
Timu ya AS Vita na TP Mzembe zinapatikana katika kundi moja na timu ya Misri Zamalek na ya Sudan Al Hilal ambazo zitachuana katika kombe la CAF litakaloanza Mei tarehe 16.
No comments:
Post a Comment