Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon |
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekaribisha kutiwa saini kwa
makubaliano ya kupatia suluhu mzozo wa Sudan Kusini, ambayo yalifanyika
mjini Addis Ababa kati ya Rais Salva Kiir na makamu wake wa zamani, Riek
Machar.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Ban amezitaka pande hizo
mbili zinazozozana kuyafanya makubaliano hayo yawe vitendo mara moja,
hususan kusitisha uhasama wote.
Katibu
Mkuu ameipongenza IGAD, hususan mwenyekiti wake, ambaye ni Bwana
Hailemariam Desalegn, Waziri Mkuu wa Ethiopia, kwa juhudi zake
zinazoendelea za upatanishi na kutafuta suluhu la amani kwa mzozo huo.
Amerejelea pia ahadi yake ya mshikamano wa Umoja wa Mataifa na watu wa
Sudan Kusini.
No comments:
Post a Comment