Maafisa zaidi ya 20 wa ngazi za juu
wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wamemuandikia barua Benjamin
Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala huo ghasibu na kumueleza kwamba jeshi
la nchi hiyo haliko tayari kupigana kwenye vita vyovyote vile. Gazeti la
Yediot Aharonot la utawala wa Israel limefichua habari hizo na kuandika
kwamba, maafisa hao wa ngazi za juu jeshini wamemueleza Waziri Mkuu ,
Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Uchumi kwamba jeshi hilo haliko tayari
kuingia kwenye vita na nchi yoyote ile. Taarifa iliyotolewa na maafisa
hao imeeleza kwamba, licha ya kupita miaka mitatu na nusu ya mazoezi
kamambe ya kijeshi lakini jeshi hilo bado halijawa tayari kuingia
vitani. Maafisa hao wamesisitiza kuwa, kujitosa kwenye vita bila ya kuwa
na maandalizi ya kutosha ni sawa na kujitangazia kifo. Maafisa hao
wameeleza kuwa, iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utaamua kuingia
kwenye vita na nchi za Kiarabu, utakabiliwa tena na fedheha iliyoukumba
mwaka 1973. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Waziri Mkuu wa Israel mara
kadhaa amenukuliwa akitoa vitisho vya kutaka kuishambulia kijeshi
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Viongozi wa Iran wamesisitiza kuwa, iwapo
utawala huo utajaribu kuleta chokochoko na kuishambulia kijeshi Iran
utakiona cha mtema kuni.
No comments:
Post a Comment