Waziri mkuu mteule Narendra Modi |
Kiongozi wa upinzani nchini India, Narendra Modi, atakuwa waziri mkuu
mpya katika taifa hilo ambalo lina historia ndefu ya demokrasia,
akishinda uchaguzi muhimu kuwahi kushuhudiwa katika nchi hiyo kwa miongo
mitatu.
Modi na chama chake cha Hindu Nationalist amekiamngusha chama cha
Congress ambacho kimekuwa kikidhibiti siasa za nchi hiyo kwa muda mrefu .Modi, ambaye ni mwanasiasa mzoefu ambaye katika kampeni yake ameahidi kuufufua uchumi wa nchi hiyo, atakuwa na mamlaka makubwa kutawala katika wakati wa mabadiliko makubwa katika jamii ya India. Pia amesema kuwa anataka kuimarisha uhusiano wa kimkakati na Marekani.
Waziri mkuu mteule Modi |
Congress yaporomoka
Matokeo yalikuwa ni kipigo kikubwa kwa chama cha Congress, ambacho kinamafungamano makubwa na ukoo wa kisiasa wa Nehru-Gandhi ambacho kimekuwa katikati ya siasa za India kwa muda wa historia ya nchi hiyo ya baada ya uhuru.
Serikali , ikiongozwa na waziri mkuu anayeondoka madarakani Manmohan Singh, imekabiliwa na kashafa za mara kwa mara za rushwa na uchumi mbovu.
Wapiga kura wa India wakisherehekea ushindi wa chama cha BJP |
"Nimekuwa nikisema kila wakati kuwa kuongoza taifa ni wajibu wetu kuwajumuisha kila mtu pamoja nasi," Modi amesema baada ya uchaguzi mrefu na uliohitaji kazi ngumu. "Nahitaji ridhaa yenu ili tuweze kuiendesha serikali ambayo inabeba kila mtu pamoja."
Ni kiongozi anayeleta mtengano
Pamoja na hayo , Modi anabaki kuwa mtu anayeleta mtengano katika nchi hiyo yenye wakaazi bilioni 1.2, kwa kiasi kikubwa kwa sababu, yeye kama waziri kiongozi wa jimbo la Gujarat, alikuwa mamlakani mwaka 2002 wakati ghasia za kikabila katika jimbo hilo ziliposababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000, wengi wao Waislamu.
Waungaji mkono wa chama cha BJP wakisherehekea |
Obama ampongeza Modi
Jana Ijumaa(16.05.2014) rais Barack Obama wa Mareakani amempigia simu Modi na kumpongeza kwa ushindi na kumwalika "kutembelea Washington katika muda ambao utakubalika na pande zote ili kuimarisha uhusiano wa mataifa yetu," Ikulu ya Marekani imesema katika taarifa.
Utawala wa Marekani ulikuwa unaangalia kunyanyuka kwa Modi kwa karibu, na mwezi Februari, kwa mara ya kwanza katika muda wa uongozi wa karne moja kama afisa wa ngazi ya juu wa jimbo la Gujarat, balozi wa Marekani alikutana nae.
Nchini India , suala sasa ni iwapo Modi anaweza kweli kuwa kiongozi anayetenganisha dini na serikali katika nchi hiyo ambayo ina waumini wa imani nyingi. Chama cha Congress kilijaribu kuibua hali ya ghasia za mwaka 2002, katika kampeni, lakini kasi ya Modi na kutoangalia sana udhaifu wa uchumi, umemfikisha katika ushindi.
No comments:
Post a Comment