Thursday 15 May 2014

Wanakijiji wawashambulia waasi wa Boko Haram

Shambulizi la Boko Haram limezuiliwa na wanakijiji kwa kuwavamia wanamgambo hao.

wanakijiji-wawashambulia-waasi-wa-boko-haramImeripotiwa kuwa shambulizi la wanamgambo wa Boko Haram lilizuiliwa na wanakijiji katika eneo la Borno.
Kwa mujibu wa maafisa wa usalama na mashahidi, washambuliaji 200 waliuawa.
Taarifa ziliarifu kuwa mpango wa washambuliaji hao kuvamia kijiji cha Kalabalge kwa silaha hatari uligunduliwa.
Afisa mmoja wa usalama alibaini kuwa wakazi wa kijiji waliaanda ulinzi baada ya habari za wanamgambo hao kupanga shambulizi kuchipuka.
Afisa huyo alileza kuwa baada ya mambambano hayo palitapakaa miili kote. Katika kijiji kimoja  kulikuwa na miili 50 na kwingine kukiwa na miili 150 ambayo yote ilidhaniwa kuwa ya wanamgambo hao.

No comments: