Friday 24 July 2015

Atletico Madrid yamsajili Mghana

Atletico Madrid yamsajili nyota wa GhanaBernard Mensah atia saini mkataba wa miaka 6 na kilabu ya Atletico Madrid

Kilabu ya Atletico Madrid kutoka Uhispania imemsajili kiungo wa kati wa Ghana Bernard Mensah kutoka kilabu ya Vitoria Guimaraes.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mtandaoni kupitia tovuti rasmi ya Atletico Madrid, Mensah alitia saini mkataba wa miaka 6 baada ya makubaliano ya usajili.


Maelezo zaidi yanaarifu kwamba Atletico Madrid imekamilisha usajili wa Mensah kwa malipo ya fedha Euro milioni 10.
Mensah mwenye umri wa miaka 20, amefunga jumla ya magoli 5 katika mechi 30 alizocheza msimu uliopita katika kilabu ya Vitoria Guimaraes nchini Ureno.
Nyota huyo wa Ghana pia anasemekana kwamba atapelekwa kuchezea Getafe kwa mkopo msimu ujao.

No comments: