Friday 31 July 2015

Mabaki ya ndege yaliyopatikana kweye ufukwe wa kisiwa cha Reunion katika Bahari ya Hind

Sehemu ya bawa ya ndege iliyopatikana ReunionMabaki ya ndege yaliyopatikana kweye ufukwe wa kisiwa cha Reunion katika Bahari ya Hindi siku ya Jumatano huwenda yakawa ni shemu ya bawa la ndege ya shirika la ndege la Malaysia Airlines iliyotoweka mwaka mmoja uliyopita kulingana na maafisa wa Malaysia na Australia.
Kugunduliwa kwa chombo hicho, ambacho kimethibitishwa na waatalamu kua ni kutoka ndege ya aina ya Boieng 777, imesababisha kuanzishwa uchunguzi mpya kutafuta ndege ya shirika la Malaysia MH370 iliyotoweka Marchi 8 2014, ilipokuwa safarini kutoka Kulalumpar kuelekea Bejing.

Waziri wa usafiri wa Malaysia Dato Sri Liow Tiong Lai, anasema "inabidi kuchunguza mabaki kabla ya kuweza kuthibitisha kwamba ni sehemu ya ndege MH370." Hata hivyo anasema ni ihara ya kwanza ya mabaki ya ndege hiyo iliyotoweka na kutojulikana imeangukia wapi.
Tume ya waatalamu wa Malaysia wameshatumwa Reunion ambako mabaki hayo yalmegundulkowa karibu na mji wa St. Andres, magharibi mwa kisiwa hicho kinachotawaliwa na Ufraransa.

No comments: