Watu hao mara baada ya kula chakula hicho ambacho kilikuwa ni
kitoweo cha nyama ya mbuzi mikate na asali walianza kutapika mfululizo
kabla ya wasamaria wema kuwakimbiza hosipitali ya rufaa ya mkoa wa
Dodoma ambapo muuguzi mfawizi wa hosipitali hiyo Rehema Mghina
akithibitisha kupokea watu hao huku akisema kuwa bado wako kwenye
utafiti wa kitabibu ili kugundua wagonjwa hao wanasumbuliwa na tatizo
gani.
Hata hiyo watu hao baada ya kulazwa kwa zaidi ya masaa 24
wameruhusiwa kurudi majumbani ambapo wameeleza kilicho wasibu mara baada
ya kula chakula hicho huku waandaaji wa sherehe hiyo wakibaki na
sitofahamu kuhusu tukio hilo.
No comments:
Post a Comment