Monday 6 July 2015

Tanzania yawatupa jela mawaziri wawili wa zamani

Tanzania yawatupa jela mawaziri wawili wa zamaniBazil Pesambili Mramba na Daniel Yona ambao walikua mawaziri katika serikali ya awamu ya tatu Tanzania, wamehukumiwa miaka mitatu jela.

Basil Mramba alikuwa ni waziri wa fedha na uchumi na Daniel Yona alikuwa waziri wa Nishati na madini wakati wa utawala wa rais Benjamini Mkapa.
Mawaziri hao wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela leo tarehe 6 mwezi Julai kwa kuisababishia serikali hasara ya bilioni 10 pamoja na utumiaji mbaya wa madaraka.
Aidha hukumu hiyo imeambatanishwa na faini ya shilingi milioni tano kwa kila mmoja wao.
Wakati huohuo, katibu mkuu wa Hazina, Gray Mgonja ameachiwa huru baada ya kutokua na hatia yoyote ile

No comments: