:Iran yakubaliana na mataifa 6 makubwa kuhusu nyuklia
Makubaliano yameafikiwa baina ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani
Baada
ya mazungumzo ya miezi kadhaa makubaliano ya kihistoria yametangazwa
kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na mataifa 6 makubwa duniani.
Mawaziri
wa mambo ya nje kutoka Iran na mataifa sita zenye nguvu duniani
wanakutana kwa mara ya mwisho huko Vienna baada ya makubaliano rasmi
kutatangazwa katika mkutano na waandishi habari.
Balozi Federica Mogherini, alipotangaza mapatano hayo
Balozi wa maswala ya kigeni wa
bara Ulaya Federica Mogherini, amechapisha mwenye mtandao wake wa
kijamii wa Twitter kuwa makubaliano kuhusiana na mradi wa kinyunklia wa
Iran yameafikiwa.
Bi Mogherini amesema kuwa ni wazi mazungumzo ya
kidiplomasia yanaweza kuleta mabadiliko makubwa ya sera kushinda
makabiliano ya kijeshi ya miongo kadhaa.
Rais wa Iran , Hassan Rouhani, amesema kuwa majadiliano hayo yamekuwa na ufanisi mkubwa Makubaliano ya kihistoria yametangazwa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na mataifa 6 makubwa duniani.
Mwandishi wa shirika la utangazaji la BBC wa masuala ya
kidiplomasia aliyeko mjini Vienna anasema kuwa licha ya matokeo ya
mazungumzo hayo kutojulikana inaonekana kuwa iran imekubali uchunguzi wa
umoja wa mataifa kukagua mipango yake ya nyuklia.
Makabuliano hayo pia yanatarajiwa kutoa ratiba ya kuondolewa kwa vikwazo vya kimataifa ilivyowekewa Iran. Rais wa Iran naye ameunga mkono mapatano hayo
Mkuu wa shirika la kudhibiti nishati ya nyuklia duniani ametoa maelezo kuhusu makubaliano yaliyoafikiwa.
Yukiya Amano amesema kuwa ''Iran imetia sahihi mpango wa kufafanua masuala yenye utata.''
Amano alisema kuwa anatarajia ukaguzi ulio kamili kwa mipango ya nyuklia nchini Iran ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Akitoa maoni yake kuhusu makubaliano hayo waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameyataja kuwa ''makosa ya kihistoria''.
No comments:
Post a Comment