Uzinduzi wa bwawa la kuvulia Pweza, Ras mzingo. Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani
NAIBU Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe:Mohammed
Said Mohammed, akizungumza jambo na watendaji wa Wizara hiyo, wakati wakati
walipokuwa wakiangalia eneo linalotaka kuvunwa Pweza huko Kisiwa Panza Wilaya
ya Mkoani.
MRATIB wa Jumuiya ya Sanaa ya Elimu ya Ukimwi na
Mazingira kisiwa Panza (JSEUMA)Juma Ali Mati, akizungumza na mmoja kati ya
wageni walioshuhudia uvunaji wa Pweza katika eneo la Kisiwa Panza.
NAIBU Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe:Mohammed
Said Mohammed,mwenye suti katikati akipiga makofi mara baada ya kukata utepe
kuashiria uzinduzi wa bwawa la kuvulia Pweza katika Ras mzingo na Ufunguo huko
Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani
WANANCHI mbali mbali wa kisiwa Panza wakielekea
baharini, kuvua Pweza mara baada ya kuzinduliwa kwa eneo lao la Ras mzingo na
Ufunguo, ambalo lilikuwa limefungwa kwa muda wa Miezi Mitatu.
VIONGOZI mbali mbali wa Serikali wakiongoza na Naibu
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe:Mohammed Said Mohammed,
katikati akiangalia wananchi wanavyovua Pweza mara baada ya kuzindua eneo la
Uvunaji wa Pweza katika Ras Mzingo na Ufungu huko Kisiwa Panza.
MMOJA wa wavuvi akirudi kuvuwa Pweza mara baada ya
eneo lao la ufugaji wa Pweza kufunguliwa huko kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani.
BAADHI ya wafanyakazi wa Idara ya Mifugo na Uvuvi
Pemba, wakimuangalia Pweza aliyevuliwa katika eneo la ufugaji lililofunguliwa
huko Kisiwa Panza
WATOTO wakimtoa Pweza kwenye shimo lake mara baada
ya kubaini kuwemo kwa Pweza katika shimo hilo, huko katika eneo la Ufugaji wa
Pweza lililofunguliwa huko kisiwa Panza.
No comments:
Post a Comment