Kamanda wa polisi wa eneo la Dodoma David Mnyambugha, alitoa maelezo na kusema kwamba ajali hiyo ilitokea nyakati za jioni wakati basi hilo lilipokuwa likisafiri kutoka Shinyanga kuelekea Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mnyambugha, basi hilo lilipoteza mwelekeo na kugonga mti na kusababisha abiria 8 kupoteza maisha papo hapo.
Abiria wengine 2 akiwemo mama mja mzito, walifariki katika hospitali moja ya mji.
Afisa mkuu wa afya wa eneo la Dodoma alisema kwamba majeruhi 27 kati ya 55 waliweza kutolewa hospitalini baada ya kufanyiwa matibabu.
Mnamo mwezi Aprili mwaka huu, watu 50 pia walifariki na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa kwenye ajali iliyowahi kutokea baada ya basi moja kugongana na lori nchini Tanzania.
Kulingana na takwimu za mwaka 2014, kumekuwa na ajali 14,048 zilizotokea Tanzania na kusababisha vifo vya watu 3,534 na majeruhi 16,166.
No comments:
Post a Comment