BAADHI ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali, waliokuwa
wakiwania nafasi ya kuteuliwa kuwa wabunge wa viti maalumu baada ya
kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu ujao, wamejikuta wakishindwa katika kura za
maoni.
Kura hizo zilizopigwa juzi na wajumbe wa mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ngazi za mikoa yote nchini, isipokuwa Mkoa wa Dar es Salaam, mbali na kuangusha baadhi ya vigogo, pia zimeibua majina mapya na kuwapa nafasi za juu, zitakazowapa fursa ya kuteuliwa kuwa wabunge wa Viti Maalumu na hata pengine uwaziri. Washindi wawili wa juu katika kura hizo katika kila mkoa, ndio walio na nafasi ya kuteuliwa kuwa wabunge wa viti maalumu, huku wa kwanza akiwa na nafasi nzuri zaidi, baada ya kupatikana kwa kura za mgombea urais wa CCM.
Miongoni mwa vigogo walioangushwa, yupo Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Shamsha Mwangunga, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana na viongozi wa mikoa wa UWT, wakuu wa wilaya na wabunge kadhaa wa Viti Maalumu wanaomaliza muda wao.
Mkoa wa Njombe
Mkoani Njombe katika kura za wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana, alijikuta akipoteza fursa ya kurejea bungeni kupitia uwakilishi wa wanawake wa mkoa huo. Mshindi katika kura hizo ni Dk Suzan Kolimba, ambaye alijizolea kura 252 na kufuatiwa na Neema Mgaya 213.
Wengine na kura zao katika mabano ni Dk Chana (164), Erika Sanga (107), Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Sitaki (38) na Magret Kyando (5).
Iringa
Katika Mkoa wa Iringa, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu na mmoja wa wenyeviti wa Bunge la 10 linalomaliza muda wake, Lediana Mng’ong’o (58) naye amepoteza fursa ya kurejea bungeni kupitia dirisha hilo la UWT.
Aliyeongoza katika kura hizo na kujihakikishia kuingia katika bunge lijalo ni Rose Tweve, aliyezoa kura 240 na kufuatiwa na Mbunge anayemaliza awamu yake ya kwanza ya ubunge huo wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati aliyepata kura 199. Mng’ong’o alijikuta akichukua nafasi ya tatu kwa kupata kura 162 na kufuatiwa na Shakira Kiwanga (89), Esta Chaula (21), Emma Mwalusamba (14), Hafsa Mtasiwa (10), Farida Ninje (4) na Agnes Nyakunga (4).
Mkoani Tabora
Katika mkoa wa Tabora, ndiko ambako wabunge waliomaliza muda wao, wamefanikiwa kutetea nafasi yao ya kurejea bungeni. Uchaguzi uliofanyika mkoani hapo, umeshuhudia Mbunge aliyemaliza muda wake, Munde Tambwe, akitetea kiti chake kwa kupata ushindi wa kwanza baada ya kuzoa kura 662. Tambwe alifuatiwa na mbunge mwenzake aliyemaliza muda wake, Mwanne Mchemba, aliyejizolea kura 342.
Wengine walioshiriki katika uchaguzi huo na kura walizopata ni Aziza Ally (290), Paskazia Malunde (52), HamidaThabit (40), Asma Suleiyum (40), Nasalile Mwaipase (16) na Agnes Mgongo (6).
Arusha
Mkoani Arusha nako, Mbunge wa Viti Maalumu anayemaliza muda wake Catherine Magige, amefanikiwa kushinda baada ya kujizolea kura 409, huku mshindi wa pili akiwa Vaileth Mfuko, ambaye alipata kura 248.
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Alphonce Kinamhala, alitaja wengine katika kundi hilo kuwa ni Flora Zelote (128), Halima Mamuya (92), Tina Timani (91), Clementina Mollel (44), Rehema Mroso (9), Nembris Kimbele (44), Catherine Sakaya (6) na Mary Morindet (51). Katika kundi la wabunge wa Viti Maalumu, aliyeshinda ni Amina Mollel aliyepata kura 362 na kumbwaga mwenzake katika kundi la walemavu, Christina Manyenye aliyepata kura (196).
Mtwara
Katika Mkoa wa Mtwara, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Anastansia Wambura aliongoza kwa kupata kura 438 na kufuatiwa na Mbunge mwingine wa Viti Maalumu anayemaliza muda wake, Agness Hokororo aliyepata kura 316. Hokororo pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma. Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Taifa, Halima Dendego, alitaja wengine walioshiriki katika uchaguzi huo na kura zao katika mabano kuwa ni Rukia Swalehe (223), Daisy Ibrahimu (204), Emma Rashid Kawawa (40), Luckiness Amlima (12), Dk Divana Kaombe (11),Asha Motto (8) na Thecla Mbuki (1).
Singida
Mkoani Singida, mbunge wa Viti Maalum anayemaliza muda wake, Diana Chilolo, alijikuta akishindwa kutetea nafasi yake baada ya kuibuka mshindi wa tatu. Mbali na Chilolo, pia msanii maarufu wa filamu, aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, ambaye alivuma wakati alipochukua fomu, naye alijikuta akishindwa katika kura hizo. Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone, alimtaja mshindi wa kwanza kuwa ni Aysha-Rose Matembe aliyezoa kura 311, huku Mbunge wa Viti Maalumu anayemaliza muda wake, Martha Mlata, akitetea nafasi hiyo baada ya kuibuka wa pili kwa kupata kura 235.
Wengine walioshiriki katika uchaguzi huo na kura zao katika mabano ni Chilolo (182), Sepetu (90), Sarah Mwambu (74), Martha Gwau (44), Rehema Madusa (24), Aziza Ntandu (5), Mary Marco (3), Sofia Joseph (2), Salome Mpondo (1), Leah Samike (1) na Elizabeth Lucas (0). Bukoba Mkoani Kagera, Mbunge wa Viti Maalumu anayemaliza muda wake, ambaye pia amekuwa Mbunge kwa miaka 25, Elizabeth Batenga ameshindwa kutetea nafasi yake.
Mbali na Batenga, pia Mbunge wa zamani wa Jimbo la Muleba Kaskazini, Ruth Msafiri, aliyekuwa akiwania kurejea bungeni kwa kupitia Viti Maalumu, naye ameanguka katika uchaguzi huo. Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo jana, Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella, alimtaja aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa huo kwa miaka mitano iliyopita, Benadetha Mshashu kuwa ndiye mshindi wa kwanza, baada ya kupata kura 432.
Mshindi wa pili ni Oliva Semguruka kutoka wilayani Ngara aliyepata kura 314. Wengine walioshiriki katika uchaguzi huo mbali na Batenga aliyepata kura 255 na Msafiri aliyeambulia kura 20 ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, Janath Kayandaali (133) na Mwagen Balaganwa (47). Pia yumo Elizabeth Ngaiza aliyepata kura 16, Levina Jovin ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa huo (16), Grace Maumbuka (7) na Domina Balyagati (7).
Morogoro Mkoani Morogoro wabunge watatu wa Viti Maalumu waliomaliza kipindi chao, Sara Msafiri, Dk Christine Ishengoma na Margaret Mkanga (Kundi la Wenyeulemavu), wametetea nafasi zao baada ya kushinda katika kura hizo. Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, aliwataja Dk Chritine Ishengoma kuwa mshindi kwa kwanza kwa kupata kura 641.
Aliyeshika nafasi ya pili ni aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia UVCCM Mkoa wa Morogoro, Sara Msafiri ambaye alichaguliwa kwa kura 608. Wagombea wengine katika kundi hilo ni Harriet Mwakifulefule, Elizabeth Lyimo, Dk Magdalena Kongera, Sarah Kalaite, Tatu Madikah, Susan Saileni, Mariam Kiamani, Mercy Minja, Redempta Mushi na Lucy Ngugi.
Katika kinyang’anyiro cha ubunge viti maalumu kwa watu wenye ulemavu mchuano, ulikuwa mkali kati ya Mbunge anayemaliza muda wake, Margaret Mkanga ambaye alipata kuwa 424 sawa na asilimia 55.99 ya kura zote 759 zilizopigwa. Mshindani wake mkubwa muigizaji wa filamu nchini, Wastara Issa alipata kura 252 sawa na asilimia 33 ya kura zote huku Chausiku Lukinga akiambulia kura 43.
Dodoma
Mkoani Dodoma, Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalli, Shamsa Mwangunga, alijikuta akishindwa kufurukuta katika uchaguzi huo, ambao Mbunge wa Viti Maalum anayemaliza muda wake, Felister Bura, aliibuka kidedea baada ya kupata kura 457. Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa (UWT) Mkoa wa Dodoma, Kaundime Kasesa, alimtaja mshindi wa pili ambaye naye ana fursa ya kuwa Mbunge wa Viti Maalumu, kuwa ni Fatma Tawfiq, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni aliyepata kura 368.
Wengine walioshiriki mbali na Mwangunga aliyepata kura 27 ni Asia Abdalah (112), Fortunata Njalala (102) na Neema Majure (78). Pia yumo Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Salome Kiwaya, Elizabeth Chagwanda, Romana Nyoni na Rahel Baragele. Wengine ni Mary Chihoma, Sarah Chwamba, Martha Dismas, Aurelia Mamboleo, Nyemo Masimba, Egla Mwamoto, Judith Muyeya, Mary Mgongo, Safina Mfaki, Mariam Ndahani, Asha Omary na Stella Mwimba.
Mikoa Mingine
Katika mikoa mingine matokeo ya awali tuliyopata ni Mkoa wa Rukwa ambao aliongoza Silafi Maufi na kufuatiwa na Bupe Mazengo;Katavi ni Taska Mbogo na Ana Lupembe; Kigoma ni Josephine Genzabuke na Philipa Mtulano; Kilimanjaro ni Shary Raymond na Betty Machangu na Tanga ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Ummy Mwalimu akifuatiwa na Sharifa Abebe.
Mkoani Mbeya mshindi ni Mary Mwanjelwa na Mary Mbwilo; Kaskazini Unguja ni Angelina Malembeka na Mwanajuma Kassim; Kusini Unguja ni Asha Msimba Jecha na Mwamtum Haji Dau; Mkoa wa Mjini ni Fakharia Khamis Shomari na Asha Abdallah Juma na Mkoa wa Mgharibi ni Tauhida Nyimbo na Kaukeb Ally Hassan.
Katika Mkoa wa Songwe, mshindi ni Juliana Shonza na Neema Mwandabila; Simiyu ni Ester Midimu na Lea Komanya; Manyara ni Martha Umbulla na Esther Mahawa huku mkoani Mara washindi ni Agnes Mathew na Christina Samo. Mkoani Ruvuma, mshindi ni Jackline Mshongozi na Sikudhani Chikambo; Kaskazini Pemba ni Maida Hamed Abdallah na Asia Sharif Omary.
Katika Mkoa wa Kusini Pemba ni Faida Mohamed na Asha Moahamed Omary huku Lindi akipita Hamida Mohamed Abdallah na Honoratha Chitanda. Katika Mkoa wa Geita, mshindi ni Vicky Kamata na Josephine Chagulla; Mwanza Kemilembe Lwota na Kiteto Koshuma; Pwani akipita Zaynab Vullu na Subira Mgalu huku Shinyanga akipita Lucy Mayenga na Azza Hilary.
Imeandikwa na Regina Kumba, Dar es Salaam, Frank Leonard, Njombe na Iringa; Lucas Raphael,Tabora; Veronica Mheta, Arusha; Abby Nkungu, Singida; Clarence Chilumba, Masasi; Angela Sebastian Bukoba; John Nditi, Morogoro na Sifa Lubasi na Grace Chilongola, Dodoma

No comments:
Post a Comment