Sunday 5 July 2015

Wabunge wengine zaidi ya 30 wafukuzwa bungeni na Spika wa Bunge

Wabunge wengine zaidi ya 30 wa kambi ya upinzani bungeni wametolewa nje ya ukumbi wa bunge na spika wa bunge Mh.Anne Makinda na kupewa adhabu ya  kutokuhudhuria vikao vitano kwa madai ya kukiuka kanuni za bunge na kutokuheshimu kiti,huku miswada mitatu ikiwasilishwa bungeni na kujadiliwa.
Mara baada ya kikao cha bunge kuanza spika wa bunge alinza kwa kuwakumbusha wabunge namna ya kufuata kanuni hasa pale wanapotaka kuondoa muswada wowote  na alipomaliza Mh.Wenje akaomba muongozo wa spika ambapo alitaka kusitishwa kwa miswada hiyo na hapo ndipo vurugu zikaanza tena lakini safari hii spika hakuahirisha bunge badala yake akawatoa nje na hapa hali ikawa hivi.
Nje ya ukumbi wa bunge wabunge hao waliotolewa nje wakazungumza na waandishi wa habari wakaelezea kitendo cha wao kutolewa nje pamoja na sababu za wao kuikataa miswada hiyo kuletwa yote pamoja na kwa hati ya dharura.
Hata hivyo baada ya vurugu zote kuisha miswada yote mitatu ambayo ni sheria ya petroli, sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi pamoja na sheria ya uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji Tanzania ambapo akiwasilisha muswada wa petroli bungeni mjini dodoma waziri wa nishati na madini Mh.Simba Chawene amesema mswada huo utajenga mfumo imara wa kusimamia sekta ya mafuta na gesi.
Wenyeviti wa kamati hizo nao wakawasilisha maoni na ushauri wa kamati zao ambapo mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini Mh. Richard Ndassa akisoma mani ya kamati amesema kamati imekubalina na serikali kuhusu mamlaka aliyopewa waziri pamoja na maoni ya wadau kuhusu kumuongezea waziri mamlaka kisheria kuingia mikataba mikubwa ya miradi ya gesi asilia pasipo kuingilia au kuwa na mamlaka sawa na TPDC

No comments: