Akisoma taarifa ya zoezi hilo mbele ya raisi Jakaya Kikwete,
aliyeungana na watanzania wa mkoa wa Pwani kwenye kujiandikisha,
mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jaji mstaafu damiani
lubuva,amesema taayari watanzania zaidi ya milioni kumi na moja
wamejiandikisha katika mikoa kumi na tatu huku matarajiwa yakiwa ni
watanzania milioni 24 wakitarajiwa, huku mikoa kumi na moja ikiwa
imesalia kukamilisha zoezi hilo.
Raisi Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa watanzania waliojitikeza
kujiandikisha katika kijiji cha Msoga Bagamoyo mkoani Pwani, kwenye
daftari la kudumu la wapiga kura zoezi lililoanza kwenye mkoa huo, na
kuipongeza tume kwa kuendelea na zoezi hilo licha ya kugubikwa na
changamoto kadha wa kadha na kutoa wito kwa watanzania kuacha kulalamika
mara baada ya uchaguzi bila ya kujitokeza kujiandikisha na kupiga kura.
Baadhi ya wananchi wa Msoga waliojitokeza kujiandikish wameelezea
changamoto ya huduma ya umeme kwaaajili ya matumizi ya mashine za BVR,
ambapo wamesema watashirikiana kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa huku
mbunge wa jimbo la Chalinze mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amewaomba
wananchi kujitokeza kujandikisha na kutumia haki yao ya msingi ya
kikatiba.
No comments:
Post a Comment