Saturday, 25 July 2015

Obama awasili Kenya kwa Kishindo kikubwa

Rais wa Marekani, Barack Obama amewasili nchini Kenya, huku kukiwa na ulinzi mkali sana, ikiwa ni mwanzo wa ziara ya siku mbili nchini humo.
Rais Obama alilakiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya. Rais wa Marekani aliepeana mikoni na viongozi wengine wa Kenya na kutia sain kitabu maalum cha wageni kabla ya kupanda kwenye gari yake.
Mitaa ya Nairobi ilikuwa imepakawa rangi na kusafishwa,  mji ulitumia kila ilichokuwa nacho kwa ajili ya kumkaribisha  Obama kwa kile ambacho wakenya wamekiita “kurejea nyumbani.”
Mkutano wa kimataifa wa wajasiriamali  wa Global Entreprenuership Summit kwa mara ya kwanza unafanyika barani Afrika. Rais Obama akiwa mmoja wa wenyeji wa mkutano huo atahutubia katika mkusanyiko  wa GES siku ya Jumamosi.
Kenya pia ina umuhimu maalum kwa rais wa Marekani. Baba yake Obama alizaliwa na kuzikwa katika eneo la vijijini magharibi mwa kenya na kutumika katika serikali wakati wa utawala wa rais wa kwanza wa Kenya.
Obama aliitembelea Kenya mwaka 2006 alipokuwa Seneta wa Marekani, lakini, hii ni ziara yake ya kwanza kama rais. Naibu rais wa Kenya, William Rutto amesema ziara hii ina maana kubwa kwa nchi yake.
“Rais Obama siyo tu kama rais mwingine yoyote wa Marekani. Ana  mizizi ya kiafrika, na ana asili ya Kenya na huu ni umuhimu kwa njia tofauti kabisa, amesema Rutto
Rais Obama akipokewa na dadake wa kambo bi Auma Obama na hata akamruhusu kusafiri naye ndani ya gari lake rasmi The Beast.

No comments: