wachezaji wa Simba wakiwa kwenye mazoezi |
Simba ina wachezaji wageni wanne ambao wana
uhakika nao tayari, hao ni Simon Sserunkuma, Hamisi Kiiza na Juuko
Murshid ambao wote ni raia wa Uganda.Pia inatarajia kumalizana na Laudit Mavugo raia wa Burundi.
Raphael Kiongera raia wa Kenya yeye ana asilimia kubwa ya kutemwa kutokana na kuwa majeruhi kwa muda mrefu.
Katika nafasi tatu ilizobakiwa nazo, mpaka sasa
majina ya wachezaji Boniface Oluoch na Michael Olunga wote wa Gor Mahia
ya Kenya, Emery Namubona wa Vital’O ya Burundi na wengine ni wachezaji
kutoka Brazil na Zimbabwe. Hao ndio walioko kwenye faili la Simba na
wanaumiza akili wakibishana nani akatwe na nani asajiliwe.
Simba inahitaji kusajili kipa, beki, kiungo na
straika ambapo sasa vigogo hao wamefanya mazungumzo na kipa wa Gor
Mahia, Oluoch ambaye pia ameonyesha nia ya kukubali na amependekezwa na
kocha wa makipa, Idd Salim. Pia Simba ipo kwenye mazungumzo na kiungo
kutoka Zimbabwe aliyependekezwa na Kocha Mkuu, Dylan Kerr.
Beki wa Vital’O, Emery tayari alifanya mazungumzo
na viongozi wa klabu hiyo na huenda akatua kwani ni mchezaji huru baada
ya kumaliza mkataba na timu yake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia
Hans Poppe, jana Ijumaa jioni alitarajia kuondoka nchini kwenda Brazili
kumfata straika mwingine. Wekundu wa Msimbazi hao wataziba nafasi ya
Kiongera na Emmanuel Okwi ambaye ameuzwa Denmark.
Juzi Poppe alisikika akisema kuwa walikuwa katika
mpango wa kuzungumza na Olunga ingawa straika huyo mwenye mabao matatu
kwenye michuano ya Kombe la Kagame na 12 kwenye Ligi Kuu Kenya (KPL)
amekanusha taarifa hizo na kwamba ana mipango yake.
“Nina mipango yangu, sijaona timu yoyote ikija
kuzungumza na mimi juu ya usajili, kikubwa nilichonacho ni kutaka
kuisadia timu yangu ifanye vizuri ndani na nje, hivyo mpango huo kwa
sasa bado sijaufikiria,” alisema Olunga kauli ambayo iliungwa mkono na
kocha msaidizi Frank aliyedai kuwa bado wanahitaji huduma ya straika
huyo.
Hata hivyo juzi Alhamis, Rais wa Simba, Evans
Aveva alifafanua akisema: “Olunga hatutamuweza, gharama yake ni kubwa
ila tuna mpango na kipa Oluoch na yeye ameonyesha nia ya kuja kwetu.”
Wakati hayo yakiendelea kwa Olunga anayewindwa na
timu tatu za jijini Dar es Salaam, Yanga, Simba na Azam, straika wa
zamani wa Yanga ambaye anacheza Sofapaka, John Baraza amemshauria Olunga
kuwa na subira ili kufanya uamuzi sahihi katika usajili wake.
Kuna taarifa klabu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini ipo tayari kutoa dola 200,000 sawa na Sh400 milioni kwa Olunga ambaye ana mkataba wa miaka minne na Gor Mahia.
Kuna taarifa klabu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini ipo tayari kutoa dola 200,000 sawa na Sh400 milioni kwa Olunga ambaye ana mkataba wa miaka minne na Gor Mahia.
Imeelezwa kwamba Kamati ya Usajili ya Simba kwa sasa haijishughulishi na usajili wa wachezaji wa ndani.
Wachezaji wapya wazawa waliosajili Simba hivi
karibuni ni Peter Mwalyanzi, Mohamed Fhaki, Samir Haji, Musa Hassan
‘Mgosi’ pamoja na Emmanuel Mtumbuka.
No comments:
Post a Comment